• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wafanya biashara Tanzania watakiwa kuweka kumbukumbu za matumizi

    (GMT+08:00) 2019-04-22 20:21:48

    Naibu Kamishna wa Kodi za Ndani katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Abdul Zuberi, amewataka wafanyabiashara kutunza risiti za manunuzi na matumizi, pamoja na kuweka kumbukumbu sahihi za matumizi mengine ambayo hayana risiti ili waweze kukadiriwa kodi stahiki.

    Zuberi amesema suala la kutunza risiti za manunuzi kwa mfanyabiashara ni jambo la muhimu kwa kuwa mfanyabiashara atapata kumbumbuku sahihi ambazo zinamsaidia wakati wa kulipa kodi.

    Zuberi alisema baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wavivu kutunza risiti za manunuzi na badala yake hulalamikia TRA kuwa inawakadiria mapato wakati hawana kumbukumbu za kuthibitisha.

    Pia alitoa elimu ya kodi pamoja na utunzaji kumbukumbu ili wafanyabiashara waweze kunufaika na serikali iweze kupata fungu lake.

    Alisema ni jukumu la TRA kuhakikisha hakuna mfanyabiashara anayefunga biashara kwa sababu ya changamoto za kodi na kwamba lengo ni kuhakikisha wafanyabiashara wote nchini wanafanya biashara na kulipa kodi stahiki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako