• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • NDONDI: Pambano la Miller na Joshua, hati hati

  (GMT+08:00) 2019-04-23 08:09:22

  Pambano la ngumi kati ya mabondia Jarrell Miller na Anthony Joshua limeingia katika utata wa kufanyika, mashabiki wao wanaendelea kutupiana vijembe.

  Pambano hilo lilipangwa kufanyika Juni mosi mjini New York Marekani lakini matatizo yalianza Machi 20 wakati taasisi ya kudhibiti matumizi ya dawa za kusisimua misuli ilimpima Miller na kumkuta na vimelea vya dawa za kusisimua misuli zilizopigwa marufuku michezoni.

  Alipohojiwa Miller amesema, ameumizwa kwa kitendo hicho na kuahidi kukata rufaa kwakuwa anadai hakuwahi kutumia dawa hizo. Leseni ya bondia huyo imesitishwa.

  Wakati hali ikiwa hivyo, mpinzani wake Joshua amesema anatafuta pambano mbadala kwakuwa alikwishaanza maandalizi na ametumia gharama kubwa kujiandaa kwa pambano hilo lililofutwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako