• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kusaidia Kenya kupata data ya ardhini kutoka angani bila malipo

    (GMT+08:00) 2019-04-23 09:23:23

    Kenya itakuwa na kituo cha kwanza barani Afrika cha kupokea data ya ardhi yake kutoka angani kupitia kwa setilaiti.

    Kulingana na makubaliano kati ya chuo kikuu cha sayansi na teknolojia cha Jomo Kenyatta JKUAT na Chuo kikuu cha sayansi cha China, data hiyo itatolewa kwa setilaiti ya Gaofen-2 ya China.

    Ronald Mutie anaripoti kutoka Nairobi ikiwa ni sehemu ya ripoti zetu mfululizo kuhusu ushikiano kati ya wasomi na wataalam wa China na Kenya.

    Ujenzi wa kituo hicho kwenye chuo cha JKUAT ni sehemu ya makubaliano ya pande mbili ambayo pia yamemepelekea kujengwa kwa maabara nyingine tano za kufanya tafiti mbali mbali.

    Lakini kabla ya ujenzi wa kituo hicho tayari serikali ya China imesaidia kujengwa kwa maabara ya kutathmini data na kutoa onyo la uwezekano wa kutokea kwa majanga.

    Profesa Hunja Waithaka ndiye mtafiti mkuu kwenye maabara hii akishirikiana na mwezake kwenye chuo kikuu cha sayansi cha China Profes Zong-Ke Zhang.

    "Malengo ya maabara hii ni kufanya utafiti na kuzalisha data kutokana na uchunguzi wa ardhi kutoka angani. Hiyo inamaanisha tunatumia picha tunazopata kutoka angani kwa ajili ya mipango na kusaidia serikali kwa mipango yake ya maendeleo. Data ya angani ni muhimu na inahitajika karibu kwenye sekta zote za uchumi ikiwemo upangaji wa anga, afya, miundo mbinu na kilimo"

    Kulingana na taakwimu kwa sasa kuna takriban satelaiti 500 kwenye obiti za dunia zikiwa umbali wa kilomita 2,000 angani.

    Na hadi sasa kuna nchi zaidi ya 50 tu zilizopeleka satelaiti katika anga la nje.

    Idadi za nchi zenye uwezo wa kuzirusha ni ndogo kwani gharama yake ni kubwa.

    Lakini kituo hiki cha pamoja kati ya Kenya na china ni afueni kubwa kwenye kanda ya Afrika Mashariki. Profesa Waithaka anasema,

    "Kupata data ya angani ni gharama kubwa na kwa hivyo tuna mpango ambapo tunashirikiana na chuo kikuu cha sayansi cha China ili kujenga kituo cha kupokea data ardhini. Kitakua kituo cha kwanza na cha aina yake barani Afrika ambapo tutaweza kupata data ya setilaiti moja kwa moja kutoka kwa mojawepo wa setilaiti za china inayoitwa Gaofen-2. Setilaiti hiyo inaweza kutuletea picha kwa chochote chenye ukubwa usiopungua mita 8. Manufaa ya mpango huu ni kwamba hatutalipa chochote. Tunaamini kwamba pindi tu tutakapopata data hii itatusaidia kama taasisi nan chi kwa jumla kuzalisha bidhaa zaidi za uvumbuzi kwenye sekta zote za uchumi wetu. Lakini pia muhimu zaidi ni kwamba data hii itachangia kuendeleza wazo na utekelezaji wa njia moja na ukanda mmoja kwa sababu data hiyo ya angani takusanywa kutoka nchi saba za Afirika mashariki ikiwemo Kenya, Uganda, Tanzania Ethiopia na sehemu ya Misri"

    JKUAT sasa inasubiri idhini kutoka kwa taasisi husika za serikali kama vile jeshi ili kuanza ujenzi wa kituo hicho.

    Kualingana na Profesa Waithaka, kitawezesha Kenya pia kupokea data kuhusu ya kusaidia uangalizi wa ardhi yake pamoja na utabiri wa hali ya hewa na kupima machafuko ya angahewa.

    "Mojawepo wa manufaa ya data ya angani ni kwamba unaweza kuona kinachofanyika na mahali kinapofanyika. Kwa mfano kwa kutumia data ya setilaiti tunaweza kuona mahali kuna ukataji wa miti msituni. Na tunaweza kuchunguza ardhi mara kwa mara na hivyo kufuatilia mabadiliko yanayotokea. Wajibu wetu kama wanasayansi ni kutoa habari kwa watunga sera husika"

    Miongoni mwa manufaa mengine kituo hicho kitasaidia Kenya kwenye ulindaji wa mazingira kwa mfano misitu na kuchunguza athari za mabadiliko ya ya tabia nchi.

    Profesa waithaka anaona kuwa kituo kipya cha pamoja kitafungua ukurasa mpya wa kuhamisha utaalam kutoka chuo kuku cha sayansi cha China ili kuwezesha Kenya kujitegemea zaidi kwenye ukusanyaji na utathmini wa data.

    "Kama nchi tunataka kutumia fursa ya ushirikiano huu ili kupata uhamisho wa teknolojia. Tunao watu hapa ambao wamepata mafunzo kuhusu uchunguzi wa ardhini kwa kutumia setilaiti lakini hatuna wataalam wenye ujuzi wa kina wa kufanya usimamizi wa data kila siku kwenye kituo cha kupokea data. Chini ya makubaliano yetu mojawepo wa waliomo ni utoaji wa mafunzo ya kusimamia kituo chetu kwa ushirikiano na wahadisi wachina."

    Chini ya ushirikiano wa JKUAT na chuo kikuu cha sayansi cha China, wanafunzi kadhaa wamepata msaada wa kwenda china kwa masomo zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako