• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na viongozi wa ujumbe wa majeshi ya majini ya nchi mbalimbali

    (GMT+08:00) 2019-04-23 14:22:37

    Rais Xi Jinping wa China leo amekutana na viongozi wa ujumbe wa nchi mbalimbali zilizoshiriki kwenye maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa jeshi la majini la China.

    Rais Xi amesema, bahari ina maana muhimu kwa maisha na maendeleo ya binadamu, na amani na utulivu wa bahari vinahusika na usalama na maslahi ya nchi mbalimbali duniani. Ameongeza kuwa watu wa China wanapenda amani, na kufuata njia ya kujiendeleza kwa amani, na jeshi la China siku zote linajitahidi kuanzisha mazingira ya usalama yenye usawa, uaminifu, na haki, ambayo yamejengwa kwa pamoja, na kuweza kunufaishana.

    Rais Xi amesisitiza kuwa jeshi la China linapenda kushirikiana na majeshi ya nchi nyingine, na kutoa mchango chanya kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa bahari.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako