• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Brela yatahadharisha wanasheria kudanganya wafanyabiashara

    (GMT+08:00) 2019-04-23 18:30:13
    Wakala wa usajili wa biashara na leseni nchini (BRELA) umewataka wanasheria ambao wanawasaidia wafanyabishara kusajili biashara zao kutowadanganya na badala yake wafuate taratibu zote na kanuni zilizowekwa na mamlaka hiyo katika usajili wa bishara.

    Mamlaka hiyo imesema kuwa licha ya wanasheria kutambuliwa kama watu sahihi kuwasaidia wafanyabishara kusajili biashara zao, wanatakiwa kufuata kanuni na taratibu zote zilizowekwa.

    Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa utawala Blera Bakari Mketo, wakati akizungumza na wafanyabishara wa mji wa Bariadi Mkoani Simiyu ambao tayari wamesajili biashara zao kwa kutumia mfumo mpya wa usajili kwa njia ya mtandao.

    Mketo alisema wamekutana na baadhi ya wafanyabishara kutoka Simiyu, ambao waliambiwa na wanasheria kuwa baadhi ya vitu havihitajiki wakati wa kusajili jambo ambalo siyo kweli.

    Kwa upande wake, Afisa kutoka Brela, Suzan Senso alisema kupitia mfumo mpya wa usajili kwa mtandao (online Registration System), watu wengi wameanza kuuelewa na kuanza kusajili biashara zao kwa kasi.

    Aliwataka wafanyabishara nchini kuendeea kusajili kwa kutumia mfumo huo, ili kuondoa usumbufu na gharama za kusajili kwenda Dar es salaam, na zaidi akiwataka kupiga simu Brela kwa ajili ya kupata ufafanuzi wowote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako