• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ushirikiano wa China na Tanzania katika utunzaji wa ziwa Tanganyika

  (GMT+08:00) 2019-04-25 08:01:31

  Kwenye mfululizo wetu wa ripoti kuhusu ushirikiano wa China na Tanzania mwandishi wetu Ronald Mutie anaripoti kuhusu ushirikiano kati ya Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi ya Tanzania Tafiri na taasisi ya jigrafia na nimnolojia ya China (Niglas).

  Ni ziwa la pili lenye kina kirefu zaidi zaidi duanini na pia mojawepo wa maziwa makubwa yenye maji safi. Linapaka na nchi nne, Tanzania, Burundi, Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na Zambia. Upepo uvuoni mwanana na eneo lote la kanda ya ziwa hupokea mvua za kutosha. Lakini pia ongezeko la watu wanaolitumia ziwa na shughuli za viwanda na kilimo vinaweza kuathiri maji na zaidi ya aina 500 ya samaki wanaopatikana humo.

  Ili kuendelea kuchunguza ubora wa maji, virutubisho na viumbe wanaoishi kwenye ziwa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi ya Tanzania Tafiri, mjini Kigoma inafanya ufuatiliaji na upimaji wa hali ya maji. Dk Ismael Aaron Kimirei ni mkurungezi wa kituo cha Tafiri mjini Kigoma.

  "Tunaangalia Kemia ya maji, tunaangalia virutubisho maji na pia tunaangalia vimelea maji, tunaangalia viroboto maji na pia tunaangalia mahitaji ya kikemikali ya ozijeni. Lakini pia tunaangalia ni kwa kiwango gani mchanga kutoka kwenye nchi kavu unavyoathiri maji na mazalia ya samaki."

  Majukumu ya Tafiri ni kufuatilia samaki kufahamu wanavyokula na pia mazingira wanayoishi. Wanaandika matokeo ya uchunguzi wao na kutoa ushauri kwa vyombo husika vya serikali ili kusaidia katika utungaji wa sera. Juhudi za Tanzania za kufanya utafiti na uchunguzi ziwani Tanzanyika pia zimepata uungaji mkono wa kimataifa. Mwaka wa 2008, taasisi ya jiografia na limnolojia ya Nanjing kutoka China (Niglas) ilisaini makubaliano ya ushirikiano na Tafiri ili kufanya uchunguzi kwenye ziwa Tanganyika, Dk. Kimirei anasema.

  "Mwaka wa 2010 wakatoa msaada wa vifaa vya maabara, pamoja na mafunzo ya kufuatilia hali ya ubora wa maji katika ziwa Tanganyika na mwaka wa 2012 walitoka tena mafunzo wakihusisha pia nchi zingine za Afrika."

  Katika maabara ya Tafiri yenye vifaa vilivyotolewa kwa msaada wa taasisi ya Niglas, Julius Asam ambaye ni mmoja wa watafiti anaendelea kupima virutubisho kwenye maji. Awali hangeweza kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa kutokana na uhaba wa vifaa, lakini sasa inamchukua muda mchache tu kufanya upimaji na kupata matokeo kamili.

  "Tulikuwa na upungufu wa vifaa lakini China wametusaidia kupata vifaa vingi kupitia kwa ushirikiano wetu wa kufanya utafiti wa virutubisho kwenye maji."

  China ikiwa ni nchi inayoendelea, inakabiliwa na matatizo pia kwenye uchafuzi wa raslimali zake za maji. Na kama vile Tanzania imeendeleza utafiti wake kwa muda mrefu ili kubaini njia za kutatua matatizo yaliopo. Dk. Kimirei ametembelea China mara nyingi na kujionea sio tu uchafuzi wa raslimali za maji lakini pia na juhudi za taasisi kama Niglas katika ufanyaji wa utafiti.

  "China inaheshimika katika tatizo hili la uchafuzi wa mazingira, lkini kwenye mafunzo yote ambayo tumepokea nchini humo, wamekuwa wakituonyesha vile uchafuzi umefanyika katika miji mbalimbali na njia ambazo wametumia kutatua baadhi ya matatizo. Kwa mfano katika ziwa la Taihu."

  Mbali na msaada wa vifaa vya maabara pia wataalam kwenye taasisi ya Tafiri wamefaidika na teknolojia mpya za ufuatiliaji na upimaji. Dk. Kimirei anasifu njia mpya waliojifunza kutoka wataalam wa China na ambayo inatumia kemikali chache lakini yenye matokeo sawa na mbinu za kawaida zilizotoka nchi za magharibi.

  "Unaweza ukakuta kwa mfano katika methodolojia ile ya nchi za magharibi, unahitaji kwa mfano mililita kumi za maji ili uweke kemikali na kusoma majibu. Lakini kwa methidolojia ya Wachina nahitaji mililita moja tu au tano na hivyo nitakuwa nimepunguza kwa nusu mahitaji ya vifaa vya maabara lakini inatupa majibu sawa na yule ambaye ametumia maji mengi na kemikali nyingi. Methodolojia hii inafaa kwa nchi maskini kwa sababu bajeti za kufanya ufuatiliaji mara nyingi ni ndogo."

  Ili kusukuma mbele ushirikiano kwenye utafiti wa maji na samaki, makao makuu ya Tafiri mjini Dar es salaam yaliwapa wataalam wa Niglas ofisi. Bibi Mary Kishe ni mtafiti mwandamizi katika taasisi ya Tafiri mjini Dar es salaam.

  "Tuliwapa vyumba viwili kwa sababu wale ni wenzetu,na lazimwa wame na mahali pa kukaa ambapo ni salama kwao. Kwa hivyo tulipata vyumba viwili, kimoja kikiwa kama ofisi na kingine kikakarabatiwa na kufanyiwa marekebisho na kuwa maabara."

  Mafanikio yaliopatikana na wataalam wa China na Tanzania kwenye utafiti wa pamoja yamechapishwa kwenye vitabu mbalimbali na pande hizo mbili zina toleo kadhaa za kazi zao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako