• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Ligi Kuu Uingereza (EPL)- Vita dhidi ya Ubingwa yapamba moto, Man City yakamata uongozi wa ligi, Arsenal yapigwa

  (GMT+08:00) 2019-04-25 09:54:54

  Kupitia migoli mitamu iliyofungwa na Bernardo Silva dakika ya 54 na la Leroy Sane dakika ya 66 imeiwezesha Manchester City jana kukwaa uongozi wa ligi kuu ya Uingereza na kufanya vita ya ubingwa wa ligi hiyo kuendelea kuwa ngumu.

  Man City imeibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Manchester United, Manchester City sasa inafikisha alama 89 baada ya ushindi huo katika michezo 35 huku Man United ikisalia na alama zake 64 baada ya kucheza mechi 34 na kuwa katika nafasi ya sita ya ligi hiyo.

  Mchezo mwingine ulikuwa kati ya washika bunduki wa jiji la London Arsenal walipokubali kipigo cha mbwa mwizi cha 3-1 toka kwa Wolverhampton Wanderers mchezo uliopigwa uwanja wa Molineux. Mabao ya Wolves yalipachikwa na Ruben Neves dakika ya 28, Matt Doherty dakika ya 37 na Diogo Jota dakika ya 45. Huku goli la kufuta machozi la Arsenal limefungwa na Sokratis Papa stathopoulos dakika ya 80.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako