• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano wa wanaviwanda wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" wafanyika Beijing

  (GMT+08:00) 2019-04-25 20:37:59

  Mkutano wa wanaviwanda wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" umefanyika leo hapa Beijing. Hii ni mara ya kwanza kwa China kuandaa mkutano kama huo wakati wa Mkutano wa kilele wa ushirikiano wa kimataifa wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja".

  Mkutano huo umeshirikisha wajumbe zaidi ya 850 kutoka China na nchi za nje wakiwemo wajumbe kutoka nchi na sehemu zaidi ya 80 duniani. Wajumbe wanaotoka nchi za nje wameeleza kuwa, pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" linatakiwa kuvishirikisha viwanda vingi vidogo na vya kati, ili kunufaisha zaidi sekta ya viwanda na biashara ya nchi mbalimbali duniani kutokana na pendekezo hilo.

  Ingawa hii ni mara ya kwanza kwa kufanyika kwa Mkutano wa wanaviwanda wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", lakini umeshirikisha idadi kubwa ya viwanda na wajumbe wa ngazi ya juu. Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya biashara ya Njia ya Hariri ya India Bw. Mansoor Nadeem Lari anasema:

  "Pendekezo la 'Ukanda Mmoja, Njia Moja' si kama tu ni mradi wa ushirikiano kati ya serikali za nchi mbalimbali, bali pia limetoa fursa kwa ushirikiano kati ya kampuni mbalimbali. Nafurahia kuona kwamba, mkutano huu wa Baraza la 'Ukanda Mmoja, Njia Moja' umetoa jukwaa hili kwa wanaviwanda, naamini kuwa utiaji saini utakaofanyika kwenye mkutano huu utaleta matokeo mengi yenye ufanisi."

  Mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha biashara cha kimataifa Bibi Arancha Gonzalez anaona kuwa, kituo hicho kikiwa mwenzi wa utekelezaji wa pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", kitatoa misaada mingi kwa viwanda vidogo na vya kati, na kuwaunganisha wawekezaji wa China na fursa zinazotolewa kutoka nchi za nje. Bi Arancha anasema:

  "Katika Maonesho ya kwanza ya uagizaji na uuzaji bidhaa nje ya China yaliyofanyika mwaka jana, tulizialika kampuni zaidi ya 100 kutoka nchi zaidi ya 20 duniani. Sasa kampuni hizo zinafanya biashara na China, na moja kati yao imeuza mazao yake ya kilimo katika maduka makubwa mbalimbali nchini China, na bado kuna mifano mingine mingi kama huu."

  Katika miaka sita iliyopita tangu pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" litekelezwe, ujenzi wa pendekezo hilo umepata mafanikio makubwa. Rais wa kundi la Standard Chartered Bw. Jose Vinals amesema, kundi hilo limefanya ushirikiano na nchi 45 zilizojiunga na pendekezo hilo, akiona kuwa pendekezo hilo litaweza kukuza masoko mapya, hasa katika bara la Asia na la Afrika, na kwamba pendekezo hilo litakuwa injini muhimu katika kuhimiza ukuaji wa uchumi duniani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako