• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kikao cha mawasiliano ya sera cha mkutano wa pili wa ushirikiano wa kimataifa wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" chapata mafanikio zaidi ya 60

  (GMT+08:00) 2019-04-25 20:07:40

  Kikao cha mawasiliano ya sera cha mkutano wa pili wa kilele wa ushirikiano wa kimataifa wa Ukanda Mmoja na Njia Moja kimefanyika leo asubuhi hapa Beijing.

  Kikao hicho kilichoandaliwa na kamati ya maendeleo na mageuzi ya taifa ya China kina kaulimbiu ya "Kuimarisha ushirikiano na maoni ya pamoja, kuhimiza maendeleo ya sifa ya juu ya Ukanda Mmoja na Njia Moja". Wageni zaidi ya 300 kutoka China na nchi nyingine 50 hivi na mashirika zaidi ya 20 ya kimataifa wamehudhuria mkutano huo.

  Kikao hicho kimepata mafanikio zaidi ya 60 ambayo ni pamoja na kutoa ripoti ya "Ujenzi wa Pamoja wa Pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja: Maendeleo, Mchango na Mustakabali" kwa lugha saba za kigeni, kusaini nyaraka za kujenga kwa pamoja "Ukanda Mmoja na Njia Moja", ushirikiano wa utengenezaji, ushirikiano wa soko la upande wa tatu na nchi kadhaa na mashirika ya kimataifa, na kuhimiza miradi mbalimbali ya ushirkiano yenye ufanisi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako