• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Xi Jinping wa China akutana na mwenzake wa Kenya Uhuru Kenyatta

  (GMT+08:00) 2019-04-25 20:14:16

  Rais Xi Jinping wa China leo amekutana na mwenzake wa Kenya Uhuru Kenyatta hapa Beijing.

  Katika mkutano wao rais Xi amesema hii ni mara ya tatu kukutana na rais Kenyatta ndani ya mwaka mmoja, ambayo inaonyesha uhusiano wa kimkakati wenye kiwango cha juu kati ya nchi mbili. Amesema China inampongeza rais Kenyatta kwa kupinga shutuma zisizo na msingi wowote juu ya ushirikiano wa China na Afrika ikiwemo Kenya. Na kusisitiza kuwa China inapenda kushirikiana na Kenya katika kulinda mwelekeo mzuri wa ushirikiano kati ya China na Afrika kwenye sekta mbalimbali, kuzidi kuunganisha mikakati, kutoa mchango wa kijamii na kiuchumi kupitia miradi muhimu ikiwemo reli, na kuhamasisha makampuni mengi ya China yawekeze nchini Kenya.

  Kwa upande wake rais Kenyatta amesema pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" linahimiza nchi mbalimbali duniani kuanzisha uhusiano wa karibu zaidi wa kibiashara na wa kiwenzi, na kuhimiza mchakato wa kuwasiliana na utandawazi wa viwanda barani Afrika. Kenya inapenda kuimarisha ushirikiano na China kwenye sekta ya ujenzi wa miundombinu, na kuimarisha mazungumzo na uratibu na China juu ya masuala ya kikanda na ya pande nyingi.

  Wakati huo huo, rais Xi Jinping wa China leo amekutana na viongozi wa nchi mbalimbali, zikiwemo Serbia, Uzbekistan, Vietnam, Mongolia, Cyprus, Belarus na Misri.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako