• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umiliki wa nyumba za bei nafuu za serikali nchini Kenya utakuwa wa bahati nasibu

    (GMT+08:00) 2019-04-25 20:44:27
    Katibu katika Wizara ya Ujenzi anayehusika na miundomsingi, Bw Charles Hinga amesema umiliki wa nyumba ambazo wakenya watakatwa pesa kwenye mishahara yao kufadhili ujenzi wa nyumba nafuu chini ya mpango wa serikali wa ajenda nne ,utakuwa wa bahati nasibu.

    Habari hii imewavunja moyo idadi kubwa ya wakenya, wakilalamika kuwa mradi huo una njama fiche na kuwa, kuna uwezekano mkubwa wa pesa za wananchi kuporwa.

    Wakenya wameshangazwa na nia ya kuwatoza pesa kwa lazima, kisha kutumia mfumo wa pata potea kugawa nyumba hizo.

    Kulingana na serikali, licha ya kuwa wafanyakazi wote rasmi watakatwa asilimia 1.5 ya mishahara kwa lazima kufadhili ujenzi huo, wafanyakazi kama hao watalazimika kutuma maombi, kukaguliwa kisha kushindana ili atakayebahatika apokezwe nyumba hiyo.

    Serikali inalenga kujenga nyumba 500,000 katika kipindi cha miaka mitatu na nusu, ingawa jumla ya wafanyakazi milioni tatu watakuwa wakikatwa pesa, pamoja na watakaojitolea kwa hiari.

    Akizungumza jana usiku katika mahojiano kwenye runinga moja hapa nchini, Bw Hinga alifichua kuwa utaratibu wa bahati nasibu utatumiwa kuamua watakaomiliki nyumba hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako