• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Mchezaji wa Burundi, Papy Faty afariki dunia Eswatini

  (GMT+08:00) 2019-04-26 08:31:36

  Kiungo wa kimataifa wa Burundi, Papy Faty amefariki ikiwa ni miezi mitatu kabla nchi yake ya Burundi kushiriki fainali zake za kwanza za kombe la mataifa ya Afrika (AFCON 2019).

  Papy alirejeshwa kwenye kikosi cha timu ya taifa hivi karibuni baada ya miaka mitatu kukosekana na jina lake likiwepo katika kikosi kitakachokwenda nchini Misri kwenye michuano hiyo ya AFCON.

  Licha ya kuonywa na daktari kuhusu matatizo yake ya moyo, Papy aliendelea kusakata kabumbu hadi jana mauti yalipomkuta baada ya kuzimia wakati akiichezea klabu yake Malanti Chiefs nchini Eswatini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako