• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na wageni wanaohudhuria mkutano wa pili wa kilele wa Baraza la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" mjini Beijing

    (GMT+08:00) 2019-04-26 08:46:32

    Rais Xi Jinping wa China jana hapa Beijing kwa nyakati tofauti amekutana na viongozi kutoka nchi 8 walioko China kuhudhuria mkutano wa pili wa kilele wa Baraza la Ushirikiano wa Kimataifa wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja".

    Alipokutana na makamu wa rais wa Indonesia, rais Xi Jinping amesema, alitoa pendekezo la "Njia ya hariri ya baharini ya karne 21" nchini Indonesia, na amefurahi kuona katika miaka ya hivi karibuni, nchi hizo mbili zimetumia fursa ya kujenga kwa pamoja "Ukanda Mmoja, Njia Moja", uhusiano kati ya pande mbili umepata maendeleo mapya.

    Alipokutana na waziri mkuu wa Papua New Guinea, rais Xi amesema, nchi hizo mbili zinajitahidi kutekeleza matokeo muhimu yaliyofikiwa kwenye ziara yake ya mwaka jana nchini Papua New Guinea, na ushirikiano na maingiliano kati ya pande mbili umepata maendeleo mapya. Amesema China inapenda kushirikiana na Papua New Guinea kuongeza uaminifu, kuzidisha ushirikiano na urafiki, na kuhimiza uhusiano kati ya nchi hizo mbili kupata maendeleo makubwa zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako