• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Maeneo ya kiuchumi yatarajiwa kufanya kazi kubwa zaidi katika ushirikiano wa kimataifa wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja"

  (GMT+08:00) 2019-04-26 09:09:57

  Maeneo ya kiuchumi na kiviwanda yamekuwa sehemu muhimu ya ushirikiano wa kimataifa kutokana na pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja".

  Kauli hii imetolewa na maofisa wa ngazi ya juu wanaohudhuria mkutano wa kilele wa Ushirikiano wa Kimataifa wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" unaofanyika hapa Beijing. Wametoa wito wa ushirikiano wa karibu zaidi kufuatia pendekezo hilo, ili kuyatumia vizuri zaidi maeneo hayo, na kuleta mafanikio zaidi ya kunufaishana.

  Waziri wa fedha wa Ethiopia Bw. Ahmed Shide amesema, maeneo ya ushirikiano ni muhimu kwa maendeleo ya sekta ya viwanda, kwani yamerahisisha biashara, na kuweza kuwa majaribio mazuri ya kuendeleza viwanda.

  Naibu waziri mkuu wa Georgia Bi. Maya Tskitishvili amesema "Ukanda Mmoja, Njia Moja" ni njia ya kufanya dunia iwe karibu zaidi, na kusema uwekezaji wa China katika maeneo ya kiuchumi ya nchi hiyo utasaidia kuendeleza uchumi na kuboresha maisha ya watu.

  Katibu mkuu wa Kamati ya Maendeleo ya Cambodia Bw. Sok Chenda Sophea ametoa wito wa ushirikiano zaidi na China kufuatia pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja".

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako