• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuimarisha zaidi ushirikiano wa kimataifa katika kulinda hakimiliki za kiubunifu

    (GMT+08:00) 2019-04-26 10:47:07

    Rais Xi Jinping wa China amesema, ili kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kulinda hakimiliki za kiubunifu kwa nguvu kubwa zaidi, China itajitahidi kuanzisha mazingira ya kibiashara yanayoheshimu thamani ya ujuzi, kukamilisha mfumo wa sheria za kulinda hakimiliki za kiubunifu kwa pande zote, na kuimarisha utekelezaji wa sheria.

    Pia China italinda vizuri zaidi maslahi ya wageni wenye hakimiliki za kiubunifu, kupiga marufuku mauzo ya lazima ya teknolojia, kulinda vizuri siri za kibiashara, na kupinga vikali vitendo vya kukiuka hakimiliki za kiubunifu kwa mujibu wa sheria. Aidha, amesema China itahimiza nchi mbalimbali duniani kufanya mawasiliano na ushirikiano wa teknolojia kwa kufuata kanuni za soko na kisheria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako