• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Miradi mbalimbali ya Mkutano wa kwanza wa Baraza la wakuu la ushirikiano wa kimataifa la "Ukanda mmoja, Njia moja" imetelezwa

  (GMT+08:00) 2019-04-26 10:47:07

  Rais Xi Jinping leo hapa Beijing amehutubia ufunguzi wa Mkutano wa kwanza wa Baraza la wakuu la ushirikiano wa kimataifa la "Ukanda Mmoja, Njia Moja".

  Katika hotuba yake, rais Xi amesema, pendekezo la kujenga kwa pamoja "Ukanda Mmoja, Njia Moja" linalenga kukusanyika pamoja katika kushirikiana na kusaidiana, na kufanya ushirikiano wa kunufaishana ili kupata maendeleo kwa pamoja. Chini ya juhudi za pamoja za pande mbalimbali, miradi mbalimbali iliyoamuliwa kwenye mkutano wa kwanza wa baraza hilo imetekelezwa vizuri, na nchi na mashirika ya kimataifa zaidi ya 150 zimesaini makubaliano ya kujenga kwa pamoja "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Pendekezo hilo limetoa fursa mpya kwa ajili ya ongezeko la uchumi wa dunia, na kuleta fursa mpya kwa ajili ya maendeleo ya nchi mbalimbali,vilevile kuanzisha mazingira mapya kwa ajili ya China kufungua mlango na kujiendeleza.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako