• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa China na Kenya wahimiza ushirikiano wa kujenga kwa pamoja "Ukanda Mmoja, Njia Moja" kupata mafanikio makubwa

    (GMT+08:00) 2019-04-26 17:07:11

    Rais Xi Jinping wa China jana hapa Beijing amekutana na rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ambaye yupo China kuhudhuria Mkutano wa Pili wa Baraza la Ushirikiano wa Kimataifa la "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Hayo ni mazungumzo rasmi ya sita kati ya viongozi wa nchi hizo mbili tangu Bw. Kenyatta alipochaguliwa kuwa rais wa Kenya mwaka 2013, na rais Xi Jinping wa China kutoa Pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Mawasiliano hayo ya mara kwa mara kati ya nchi hizo mbili yamehimiza kwa nguvu ushirikiano wenye ufanisi kati ya pande hizo mbili katika kujenga kwa pamoja "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na kupata mafanikio mazuri.

    Mwezi Agosti mwaka 2013, viongozi wa nchi hizo mbili walikutana kwa mara ya kwanza, na kupanga kwa pamoja matarajio na hatua za kuhimiza ushirikiano wa kusaidiana na kunufaishana. Mwezi Desemba mwaka 2015, ujenzi wa reli ya SGR ambayo ni reli ya kwanza iliyojengwa kwa kufuata kigezo cha kichina barani Afrika ulianza nchini Kenya, na kukamilika ndani ya miaka miwili, na umetoa nafasi elfu 50 za ajira kwa wananchi wa huko, na kuleta mapato ya dola za kimarekani milioni 100.

    Mwezi Desemba mwaka 2015, viongozi hao wawili walikutana kwa mara ya pili wakati wa Mkutano wa viongozi wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika. Rais Xi ameeleza kuwa pande hizo mbili zinatakiwa kuimarisha mawasiliano ya utamaduni, na kuhimiza utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo Kituo cha utafiti wa pamoja kati ya China na Afrika. Kituo hicho kimekabidhiwa kwa Kenya ndani ya miaka miwili. Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2018, kituo hicho kimeanzisha ushirikiano na mashirika 20 ya sayansi na elimu ya Kenya, Tanzania na Ethiopia, kuzindua miradi 45 ya utafiti wa pamoja, na kuandaa wataalamu zaidi ya 280 kwa nchi mbalimbail za Afrika.

    Katika miaka ya hivi karibuni, mazungumzo kati ya viongozi wa nchi hizo mbili yamekuwa yakiimarishwa. Rais Xi pia ametoa ahadi ya kupanua uagizaji wa bidhaa kutoka Kenya, hali inayoonesha nia ya China ya kutatua tatizo la kutokuwepo kwa uwiano wa kibiashara kati ya pande hizo mbili, ili kuzifanya bidhaa za Kenya kufahamika na kukaribishwa na watu wa China.

    Wakati wa Mkutano wa pili wa Baraza la ushirikiano wa kimataifa la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" unaoendelea mjini Beijing, viongozi wa nchi hizo mbili wamekutana tena mjini Beijing. Tunaamini kuwa kutokana na msukumo wa viongozi hao, ushirikiano kati ya pande hizo mbili katika sekta mbalimbali utapata mafanikio makubwa zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako