• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Kenya asema, ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" unatarajiwa kukuza zaidi ushirikiano wa kibiashara kati ya Kenya na China

    (GMT+08:00) 2020-02-26 13:03:31

    Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" unatarajiwa kutoa msukumo mpya kwa ushirikiano wa kibiashara kati ya Kenya na China na kuwaletea manufaa wananchi wa nchi zote mbili.

    Rais Kenyatta ameyasema hayo leo hapa Beijing wakati akihutubia Mkutano wa Kuvutia Uwekezaji kutoka China Kwenda Kenya uliofanyika kando ya Kongamano la Pili la Kilele la Ushirikiano wa Kimataifa la "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Rais Kenyatta amesema Kenya na China zimedumisha mwelekeo mzuri katika kufanya ushirikiano wa kusaidiana na kunufaishana chini ya pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na hivi sasa baadhi ya miradi ya ushirikiano imepata faida, baadhi iko mbioni kujengwa na kuna mingine itatekelezwa taratibu.

    Anasema,  "Jana nilikuwa na mazungumzo ya kiujenzi na rafiki yangu na mshirika wangu Rais Xi Jinping wa China. Kwenye mazungumzo yetu tulikubaliana kuimarisha ushirikiano wa nchi zetu kwenye sekta ya uwekezaji, na kuhakikisha ushirikiano wa miundombinu unaweza kuvutia uwekezaji mwingi, kuongeza nafasi za ajira, kuchochea maendeleo ya uchumi nchini Kenya, na pia kuhimiza tija kwenye uzalishaji katika hali ya kunufaishana. Nafurahi sana kuwaona wawekezaji wengi wa China wanashiriki kwenye mkutano huu wa leo, kwani kuja kwenu ni ushahidi wa nia ya China na wawekezaji wa China kufanya ushirikiano wa kibiashara na kuwekeza nchini Kenya"

    Rais Kenyatta amesema Kenya inatarajia kutumia fursa ya Kongamano la Pili la Kilele la Ushirikiano wa Kimataifa la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" kuwavutia wawekezaji wa kichina kwenda kuwekeza nchini Kenya kufuatia kanuni ya kimsingi ya kunufaika kwa pamoja na pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na kushirikiana na Kenya kujenga mustakabali mzuri wa kupata mafanikio ya pamoja.

    Anasema, "Tunachotaka sio tu wawekezaji wa kichina kuja Kenya kutusaidia, bali pia mnakuja kuwekeza na kuchuma pesa nchini kwetu. Mkipata pesa, sisi pia tutapata pesa; mkipata pesa, tutaongeza nafasi za ajira; na mkipata pesa, tutapata maendeleo. Kwani tukifanya hivyo lengo la kunufaika kwa pamoja na matunda ya pendekezo la 'Ukanda Mmoja, Njia Moja' litaweza kutimizwa. Naona hii ndiyo kiini cha pendekezo hilo katika kupanua mawasiliano, biashara na uwekezaji duniani. Tunatarajia kuwa nyinyi mnaweza kupata manufaa katika mchakato huo. Karibu Kenya, tujitahidi kwa pamoja!"

    Mkutano wa Kuvutia Uwekezaji kutoka China Kwenda Kenya uliandaliwa na Wizara ya Viwanda, Biashara na Ushirikiano ya Kenya na Ubalozi wa Kenya nchini China, na unalenga kuhimiza ushirikiano wa kibiashara na kutoa fursa ya mawasiliano kati ya makampuni ya nchi hizo mbili ili kuongeza maelewano ya kampuni za China kuhusu mazingira ya kibiashara na sera nafuu katika sekta za kilimo, uzalishaji viwandani, matibabu na afya, nyumba na ujenzi wa miundombinu nchini Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako