• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri wa uchukuzi wa Kenya atarajia makampuni mengi zaidi ya China kuwekeza nchini Kenya

  (GMT+08:00) 2019-04-27 10:49:26

  Mkutano wa baraza la uwekezaji kati ya China na Kenya umefanyika leo hapa Beijing na kuhudhuriwa na maofisa waandamizi wa Kenya akiwemo Rais Uhuru Kenyatta na jumuiya ya wafanyabiashara na wawekezaji wa China.

  Mkutano huo uliofanyaika pembeni ya mkutano wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", umekuwa ni fursa nzuri ya kutangaza vivutio vya Kenya kwa wawekezaji wa China. Waziri wa uchukuzi wa Kenya Bw. James Macharia aliendesha mkutano huo na kueleza maoni yake kuhusu jinsi mkutano uliofanyika.

  "Wachina wengi hasa wafanya biashara wanaofanya kazi hapa China na Kenya, na wengine wanapenda kuja Kenya kwa kuwa wanafahamu kuwa Kenya kuna fursa nyingi za biashara. Tunajua kuwa katika miaka kumi iliyopita kumekuwa na uwekezaji mwingi kutoka China, kama kwenye ujenzi wa barabara. Wanakuja na raslimali, mashine na pesa kutusaidia kujenga barabara kubwa. Reli SGR ni mfano mzuri, kwani iliweza kukamilika miezi 18 kabla ya wakati, na imetusaidia sana wakenya kiuchumi. Kwa hiyo yakija makampuni zaidi kutoka China, tutafurahi zaidi na gharama zetu kwenye ujenzi zitakuwa chini."

  Licha ya kuwa mradi mkubwa zaidi unaotajwa na kufahamika zaidi kati ya miradi "Ukanda Mmoja, Njia Moja" ni reli ya SGR na awamu zake mbili, Waziri Macharia amesema kuna miradi mingi inayohusu "Ukanda Mmoja, Njia Moja" inayoendelea nchini Kenya, mbali na reli ya SGR.

  "Kuna miradi mingi sana kwenye shoroba za kiuchumi, kuna mabarabara Mombasa, kuna barabara Nairobi, kuna barabara ya magharibi na barabara kuu ya Nairobi itakayosaidia kupunguza msongamano wa magari, kuna bandari ya Kisumu, na hata kuna eneo maalum la viwanda, kuna miradi mingi tu.

  Mapema asubuhi ya leo Rais Uhuru Kenyatta alihutubia mkutano huo, na kutangaza kuwa Kenya itaendelea kuboresha zaidi mazingira yake ya uwekezaji, na kukaribisha wawekezaji zaidi kutoka Kenya ili kuongeza ajira, na kuhimiza utekelezaji wa ajenda ya serikali ya Big Four.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako