• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano wa wakuu wa Baraza la ushirikiano wa kimataifa la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" wafanyika

  (GMT+08:00) 2019-04-27 13:10:10

  Mkutano wa kilele wa baraza la wakuu la ushirikiano wa kimataifa la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" umefanyika leo asubuhi, na kuhudhuriwa na viongozi 37 wa nchi, maofisa wa Umoja wa Mataifa na wa Shirika la Fedha la Kimataifa IMF.

  Rais Xi Jinping wa China ameendesha mkutano huo na kutoa hotuba ya kufungua mkutano huo "Kujenga kwa pamoja 'Ukanda Mmoja, Njia Moja' kwa sifa bora ".

  Amesema, China inatumai kushirikiana na pande mbalimbali, ili ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" uendelezwe kwa kina zaidi, na kuwanufaisha zaidi watu wa nchi mbalimbali.

  Ametoa mapendekezo matatu ya kujenga "Ukanda Mmoja, Njia Moja" kwa sifa bora, kwanza kwa kushirikiana na pande mbalimbali kukamilisha wazo la ushirikiano na kuzingatia kujenga "Ukanda Mmoja, Njia Moja" kwa sifa bora. Pili, kushirikiana na pande mbalimbali kuhakikisha sekta zinazotiliwa maanani kwenye ushirikiano, kutoa kipaumbele kuimarisha mawasiliano katika pande zote. Tatu, kushirikiana na pande mbalimbali, kuimarisha mfumo wa ushirikiano, kuzingatia kujenga uhusiano wa kiwenzi unaoungana.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako