• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa pili wa "Ukanda Mmoja Njia Moja" wamalizika

    (GMT+08:00) 2019-04-27 20:35:02

    Mkutano wa pili wa baraza la kimataifa la ushirikiano wa "Ukanda mmoja, Njia moja" umemalizika leo hapa Beijing. Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika baada ya kufungwa kwa mkutano huo, Rais Xi Jinping wa China amesema, jumla ya vipengele 283 vya matokeo ya kiutendaji vimefikiwa makubaliano kwenye mchakato kuanzia maandalizi na wakati wa mkutano huo, ambapo mikataba ya miradi yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 64 ilisainiwa wakati wa kikao cha wanaviwanda.

    Rais Xi alisema,  "Viongozi wa nchi mbalimbali na mashirika ya kimataifa walifanya mjadala kwa kina, na kufikia maoni ya pamoja katika kutekeleza kwa ufanisi pendekezo la 'Ukanda Mmoja Njia Moja', vile vile tumekamilisha dhamira ya ushirikiano, maeneo yanayopewa kipaumbele na mfumo wa ushirikiano wetu. Hayo yote yatakuwemo kwenye taarifa ya pamoja ya mkutano huu na kuelekeza ushirikiano wa kimataifa katika juhudi za kujenga kwa pamoja 'Ukanda Mmoja, Njia Moja' katika siku zijazo."

    Kuhusu matunda ya mkutano huo, rais Xi alifafanua kwamba vipengele 283 vya matokeo ya kiutendaji vimefikiwa makubaliano, ambavyo ni pamoja na ushirikiano kati ya serikali, miradi halisi ya ushirikiano, kuanzisha jukwaa la ushirikiano wa pande zote katika fani mbalimbali, kutoa taarifa ya maendeleo kuhusu kujenga kwa pamoja "Ukanda Mmoja Njia Moja" na taarifa ya kamati ya kutoa mapendekezo ya kisera ya baraza hilo. Katika nafasi ya nchi mwenyekiti wa baraza hilo, China itaandaa na kutangaza orodha ya matunda ya mkutano huo. Vile vile katika kikao cha wanaviwanda kilichoandaliwa wakati wa mkutano huo, mikataba ya miradi yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 64 ilisainiwa.

    Rais Xi aliongeza kuwa, viongozi waliohudhuria mkutano huo wamekubaliana kuwa, kujenga kwa pamoja "Ukanda Mmoja Njia Moja" ni hatua ya kuelekea ustawi wa pamoja, ambayo inatoa fursa ya kupata maendeleo kwa nchi mbalimbali, na jukwaa la kuimarisha ushirikiano wa kimataifa. Rais Xi Jinping alisisitiza kuwa, katika kutekeleza pendekezo la "Ukanda Mmoja Njia Moja", inafuatwa kanuni ya pande zote kufanya mashauriano kwa usawa, kubeba majukumu kwa pamoja na kupata manufaa kwa pamoja, ndiyo maana nchi yoyote inakaribishwa kujiunga na shughuli hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako