• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Hotuba aliyotoa Rais wa China kwenye ufunguzi wa Baraza la Ukanda Mmoja Njia moja yapata mwitikio mkubwa katika jumuiya ya kimataifa

  (GMT+08:00) 2019-04-28 10:08:44

  Rais Xi Jinping wa China alitoa hotuba kuhusu "Kushirikiana kwa pamoja katika kujenga mustakbali mzuri wa 'Ukanda mmoja, Njia moja'" kwenye ufunguzi wa mkutano wa pili wa kilele wa Baraza la ushirikiano wa Ukanda mmoja njia moja uliofanyika Ijumaa hapa Beijing. Hotuba hiyo imepata mwitikio mkubwa kwenye jumuiya ya kimataifa.

  Pande mbalimbali zinaona kuwa, mitizamo aliyotoa rais Xi Jinping kwenye hotuba hiyo kuhusu kujenga mahusiano ya wenzi wa mafungamano ya kimataifa na kuimarisha ushirikiano wa kuhimiza maendeleo ya kimataifa, inasaidia kuhimiza ushirikiano wa kiutendaji kwenye nyanja mbalimbali, kupanua maslahi ya pamoja, na kutoa mchango mkubwa zaidi katika kujenga Jumuiya ya bindamu yenye hatma ya pamoja.

  Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha usimamizi na utafiti wa sera katika Jumuiya moja ya washauri bingwa nchini Zambia Bi. Bernadette Deka-Zulu amsema, pendekezo la Ukanda mmoja, Njia moja limeweka jukwaa jipya la kuhimiza biashara na uwekezaji wa kimataifa, ambalo limeunganisha dunia nzima kwa kupitia ujenzi wa miradi mbalimbali ya miundombinu, na kuipatia Afrika fursa ya kujiunga kwenye mfumo wa biashara duniani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako