• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ujenzi wenye sifa nzuri wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" kuleta manufaa mengi

  (GMT+08:00) 2019-04-29 16:57:13

  Mkutano wa pili wa kilele wa ushirikiano wa kimataifa wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" umefungwa hapa Beijing, na makubaliano zaidi ya 280 yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 640 yamefikiwa. Wataalam wanaona kuwa, ujenzi wa pamoja wenye sifa nzuri wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" utaweza kutimiza lengo la kuunganisha ufanisi wa uchumi, jamii na uhifadhi wa mazingira.

  Mkutano wa kwanza wa kilele wa ushirikiano wa kimataifa wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" uliofanyika mwaka 2017, ulifikia makubaliano mengi, na baadaye pande zinazohusika zilitekeleza hatua mbalimbali na kupata mafanikio mengi halisi. Mkutano huu wa pili ni mkubwa zaidi. Mtafiti wa Taasisi ya Mikakati ya Kitaifa ya Chuo Kikuu cha Qinghua Bw. Ding Yifan anasema,

  "Kwenye mkutano huu, ni dhahiri kwamba pendekezo la 'Ukanda Mmoja, Njia Moja' limekaribishwa zaidi na nchi nyingine, kwani limeshirikisha nchi nyingi zaidi, na kuwa na ushawishi mkubwa zaidi. Safari iliyopita pande mbalimbali zilijadili nia ya ushirikiao, lakini mara hii, zimezungumzia namna ya kutekeleza makubaliano na kulisukuma mbele zaidi pendekezo hilo."

  Kwenye mkutano wa mwaka huu, rais Xi Jinping wa China alitangaza kuwa, China itachukua hatua muhimu mbalimbali za mageuzi na kufungua mlango, kwa kupunguza sekta zisizoruhusu kuwekezwa na wawekezaji wa nje, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kulinda hakimiliki za kiubunifu, kuongeza maagizo ya bidhaa kutoka nchi za nje, kutekeleza uratibu wa sera za uchumi wa kimataifa kwa ufanisi zaidi, na kutilia maanani zaidi utekelezaji wa sera ya mageuzi na kufungua mlango. Bw. Ding anaona kuwa, hali hii imeonesha nia ya China ya kufungua mlango zaidi, na pia imeondoa wasiwasi wa nchi nyingine kuhusu maendeleo ya China.

  Jambo lingine linalofuatiliwa zaidi ni kuwa, rais Xi pia amedhihirisha malengo ya ujenzi wa pamoja wenye sifa nzuri wa pandekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na mwelekeo wa ushirikiano wa pendekezo hilo. Wataalam wanaona kuwa, makubaliano yaliyosainiwa kwenye mkutano huo yametoa ishara ya kuhimiza maendeleo yenye sifa nzuri. Naibu mkurugenzi wa Kamati ya Sera ya Uchumi ya Taasisi ya Utafiti wa Sayansi ya Siasa ya China Bw. Xu Hongcai anasema,

  "Kiini cha mkutano huo ni kuhimiza ushirikiano wenye sifa nzuri. Hivyo inapaswa kuunganisha ufanisi wa uchumi, ufanisi wa jamii na uhifadhi wa mazingira kwa njia bora, kwa kufuatia utaratibu wa kimataifa na uzoefu mzuri wa nchi zilizoendelea."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako