• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Serikali za Tanzania kusajili laini za simu

    (GMT+08:00) 2019-04-29 19:47:10

    Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Mashariki, Lawi Odioro amesema zoezi la usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole halitaathiri huduma za kifedha zinazotolewa na mitandao ya simu na kwamba kwa sasa wameamua kutoa elimu kuhusu zoezi hilo ili kuwatoa hofu wananchi.

    Kabla ya zoezi hilo, wananchi wamekuwa wakisajili kwa kutumia vitambulisho mbalimbali ikiwemo kadi ya mpiga kura hata hivyo bado kumekuwa na matukio ya uhalifu kwa njia ya mtandao.

    Mhandisi Odioro amesema kuwa lengo la kuendesha zoezi la usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole ni kudhibiti vitendo vya uhalifu unaofanywa kwa njia ya mitandao ukiwepo utapeli hivyo aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kusajili laini zao za simu ifikapo Mei Mosi ingawa zoezi hilo litamalizika Desemba 31 mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako