• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Dijk, mchezaji bora wa mwaka wa PFA, Vivianne ashinda kwa wanawake.

  (GMT+08:00) 2019-04-30 10:06:39

  Beki wa Livepool Virgil Van Dijk ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa chama cha wachezaji wa kulipwa Uingereza (PFA).

  Libero amekuwa beki wa kwanza kutwaa tuzo hiyo tangu nahodha wa zamani wa Chelsea na Uingereza John Terry alipotwaa tuzo hiyo mwaka 2005.

  Dijk amewapiku mastaa Sadio Mane, Sergio Aguero, Raheem Sterling wa Manchester City alikuwa mpinzani wake mkubwa katika kuwania tuzo hizo, Edin Hazard na Bernardo Silva.

  Wachezaji wengine wa Liverpool, Mane, Andy Robertson na Trent Alexander wamechaguliwa katika kikosi bora cha mwaka cha nyota 11.

  Kwa upande wa wanawake, mwanadada wa washika bunduki wa jiji la London Arsenal, Vvianne Miedema amenyakua tuzo hiyo ya mwanasoka bora wa mwaka.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako