• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping atoa wito kwa vijana wa China

    (GMT+08:00) 2019-04-30 13:57:29

    Mkutano wa kuadhimisha miaka 100 ya Vuguvugu la Mei 4 umefanyika leo hapa Beijing.

    Akihutubia mkutano huo, rais Xi Jinping wa China amesema, kutafuta ustawi wa taifa ni wajibu wa vijana, vijana katika zama mpya wanatakiwa kuwa wenye bidii, watangulizi, na wajitolea, na kufanya juhudi katika kujifunza elimu ili kuzifanya mitazamo, mawazo na kiwango cha utambuzi zao kukidhi mahitaji ya maendeleo yanayopiga hatua kwa kasi. Pia amesisitiza kuwa ujenzi wa nchi yenye nguvu katika mambo ya kisasa ya ujamaa unategemea uwezo mkubwa wa kifedha, na pia imani imara ya watu. Rais Xi vilevile ametoa wito kwa kamati za chama na serikali katika ngazi mbalimbali pamoja na jamii nzima kufanya mawasiliano ya ana kwa ana na vijana, kusikiliza maoni na mapendekezo yao juu ya kazi za chama na serikali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako