• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China ahamasisha vijana wa China kwenye hotuba yake ya kuadhimisha Siku ya Vijana

  (GMT+08:00) 2019-04-30 17:21:36

  Kabla ya kufika kwa Siku ya Vijana ya China ambayo ni tarehe 4, Mei, mkutano mkubwa wa hadharaumefanyika leo hapa Beijing, ili kuadhimisha miaka 100 tangu kufanyika kwa Harakati ya Tarehe 4, Mei. Rais Xi Jinping wa China amehutubia mkutano huo akiwahamasisha vijana wawe na uzalendo, upendo kwa familia na binadamu wote, pia amewataka wafanye juhudi ili kutimiza ustawishaji mpya wa taifa la China, na ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.

  Mwaka 1919, kutokana na udhaifu wa serikali ya Beiyang ya China ambayo ni mshindi kwenye Vita vikuu vya kwanza vya Dunia, kwenye mkutano wa Amani wa Paris, nchi za magharibi ziliamua kutoa mamlaka ya ukoloni ya Ujerumani kwenye mji wa Qingdao, China kwa Japan. Hali hii iliwakasirisha sana wachina. Tarehe 4, Mei mwaka huo, baadhi ya vijana walianzisha harakati ya kizalendo kote nchini China, na kuleta mawazo ya Umarx. Harakati hiyo ndiyo Harakati maarufu ya Tarehe 4, Mei ya China.

  Rais Xi anaona kuwa harakati hiyo si kama tu ni harakati ya mapinduzi ya kijamii na kiutamaduni, bali pia ni mwanzo wa ustawishaji mpya wa taifa la China. Amesema kupitia harakati hiyo, vijana wa China waligundua nguvu yao kubwa, na uzoefu wa miaka 100 iliyopita umethibitisha kuwa wao ni vijana wenye matumaini makubwa, uzalendo na uwezo wa uvumbuzi, na siku zote ni watangulizi wa ustawishaji mpya wa taifa la China.

  Huu ni mwaka wa 100 tangu Harakati ya Tarehe 4, Mei ya mwaka 1919 ifanyike, pia ni mwaka wa 70 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China. Hivi leo China imekuwa nchi ya pili kwa nguvu ya uchumi, na kuagana kabisa na udhaifu na fedheha zilizoikumba nchi hiyo miaka 100 iliyopita. Lakini mchakato wa kutimiza ustawishaji mpya wa taifa la China bado unahitaji juhudi za vijana. Hivyo rais Xi amewataka vijana wa China wasiache moyo wa kufanya kazi kwa bidii. Kwa kweli, vijana wa China wamerithi desturi nzuri ya kufanya kazi kwa bidii. Kutoka vijana wa kupeleka vifurushi hadi wafanyakazi vijana wa teknolojia ya anga ya juu, vijana wa China wanatengeneza mwujiza wa maendeleo unaoshangaza dunia nzima.

  Gazeti la New York Times la Marekani lilitoa ripoti ya "Suala kubwa la dunia: Vijana", na kutahadharisha viongozi wa nchi mbalimbali duniani kuwa, lisiposhughulikiwa vizuri suala la vijana, dunia haitakuwa na mustakabali mzuri. Rais Xi anatilia maanani sana suala hilo, na kuona kuwa, "ustawi wa vijana huleta ustawi wa taifa, na nguvu ya vijana ni nguvu ya nchi". Kati ya miradi 26 ya ushirikiano iliyofikiwa kwenye mkutano wa pili wa kilele wa ushirikiano wa kimataifa wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" uliofanyika hivi karibuni hapa Beijing, miradi 5 inawahusisha vijana.

  Kuwafundisha vijana wa China wawe wajenzi hodari wa Ujamaa wenye Umaalumu wa China, ni muhimu kwa majukumu muhimu ya kimkakati ya China. Rais Xi amesema, kujenga China iwe nchi yenye nguvu kubwa ya kijamii, na kutimiza ustawishaji mpya wa taifa la China ni safari ndefu, na anatumai vijana wa China watakuwa na matokeo mazuri kwenye safari hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako