• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mashirika makubwa ya serikali Kenya hatarini kupigwa mnada kutokana na madeni

    (GMT+08:00) 2019-04-30 19:49:25

    Huku serikali ikiendelea kuomba mikopo zaidi nchini China, mashirika yake manane makuuu yako katika hatari ya kupigwa mnada kuwa kushindwai kulipa jumla ya Sh147.7 bilioni ambazo ilikuwa imekopa kutoka nje kufikia Desemba, 2018.

    Kulingana na ripoti ya Idara ya Utayarishaji wa Bajeti Bungeni (PBO) iliyowasilishwa Alhamisi kwa Kamati ya Bunge kuhusu Bajeti, mashirika ambayo mali yao yako katika hatari ya kuuzwa ni; Kampuni ya Kusambaza Umeme Nchini (Kenya Power) inayodaiwa Sh14.02 bilioni, Shirika la Ndege Nchini (KQ) 76.39 bilioni, Halmashauri ya Bandari Nchini (KPA) Sh33.7 bilioni, Kampuni ya Kuzalisha Umeme Nchini (KenGen) Sh10.86 bilioni. Shirika la Utangazaji Nchini (KBC) Sh6.95 bilioni.

    Mashirika mengine yanayodaiwa ni; Shirika la Reli Nchini (KR) Sh4.59 bilioni, Halmashauri ya Ustawi wa Mito ya Tana na Athi (TARDA) Sh542 milioni na Kampuni ya kutengeneza Saruji, East African Portland Cement Sh674 milioni.

    Ripoti hiyo inasema mali ya mashirika hayo yalitumiwa na serikali kama dhamana kwa mikopo iliyopata kutoka kwa China na Kitengo cha kufadhili maendeleo kimataifa katika Benki ya Dunia (WB). Wizara ya Fedha ilisema deni la Kenya linakisiwa kufikia Sh5.6 trilioni itimiapo Juni mwaka huu. Na mzigo huo wa deni unatarajiwa kupanda hadi Sh7 trilioni ifikapo 2022 Rais Uhuru Kenyatta atakapokuwa akiondoka mamlakani baada ya kukamilisha kipindi chake cha pili na cha mwisho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako