• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • ATE kutoa tuzo kwa mwajiri bora

    (GMT+08:00) 2019-04-30 19:50:09

    Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), kimezindua rasmi mchakato wa kumtafuta mwajiri bora wa mwaka huu lengo likiwa ni kutambua mchango wa waajiri wenye misingi bora ya usimamizi wa nguvu kazi na rasilimali watu ili kuwawezesha kutimiza wajibu wao kwa ajili ya kuongeza uzalishaji kibiashara.

    Mkurugenzi Mtendaji wa ATE, Dk. Aggrey Mlimuka, amesema tuzo ya mwajiri bora wa mwaka (EYA) ni zoezi lililoanzishwa na kuendeshwa kila mwaka na Chama cha Waajiri Tanzania tangu mwaka 2005.

    Alisema ushiriki wa tuzo ya mwajiri bora umeendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka kutokana na ukweli kuwa waajiri wengi wamehamasishwa kuthamini watu katika kufanikisha shughuli za biashara kama nyanja muhimu ya usimamizi wa rasilimali watu mahali pa kazi.

    Dk. Mlimuka alisema mwaka huu 2019 kutokana na maoni waliyopokea kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, wadau na wataalamu wetu mbalimbali, tuzo ya mwajiri bora kwa mwaka huu wameongeza vipengele vipya vitatu na kufikia vipengele 38 kutoka 35 vilivyokuwapo awali.

    Alivitaja vipengele vilivyoongezeka kuwa ni mwajiri bora anayeendeleza mafunzo ya ujuzi wa kazi kwa wahitimu (Internship), Mwajiri bora anayetoa mafunzo ya Uanagenzi na Mwajiri Bora anayezingatia hakirasilimali (local content).

    Alisema mchakato wa kumpata mwajiri bora wa mwaka huwa una sehemu mbili ya kwanza ni ya utafiti itakayofanya kupata washindi na kwa sasa sehemu hiyo ipo chini ya kampuni binafsi ya TanzConsultinayoongozwa na Prof. BAT Kundi, na sehemu ya pili ni usimamizi wa matukio mpaka kilele cha sherehe ambacho kimepangwa kufanyika Desemba, mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako