• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda yaahidi kufanya vizuri michuano ya Baseball Afrika

    (GMT+08:00) 2019-05-01 10:38:48
    Michuano ya mchezo wa Baseball Afrika inaanza leo jijini Johannesburg Afrika Kusini, huku mataifa ya Afrika Kusini ambao ni wenyeji wa michuano hiyo, sambamba na Uganda, Nigeria. Burkina Faso na Zimbabwe zitashindania ubingwa huo wa Afrika.

    Timu ya Uganda imewasilia jana usiku nchini humo tayari kupeperusha bendera ya Uganda katika michuano hiyo huku kocha wa timu hiyo Katsuhisa Tanaka ameweka wazi ari waliyonayo ya kuondoka na kombe hilo.

    Bingwa wa michuano hiyo atawakilisha bara la Afrika katika mashindano ya kufuzu michuano ya Olimpiki kati ya Ulaya na Afrika yatakayoanza Septemba 18 hadi 22 nchini Italia kabla ya kuelekea michezo ya Olimpiki itakayofanyika mwakani nchini Japan.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako