• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wachina watalii katika mapumziko ya sikukuu ya Mei Mosi

  (GMT+08:00) 2019-05-01 18:08:30

  Mapumziko ya sikukuu ya Mei Mosi ya mwaka huu yamerefushwa na kuwa siku nne kutoka siku tatu, na kuwawezesha wachina wengi zaidi kutalii.

  Sikukuu ya Mei Mosi iko katika majira ya mchipuko, na kila mwaka katika mapumziko ya sikukuu hiyo, wachina wengi hutalii katika sehemu mbalimbali nchini China na hata nje ya nchi. Inakadiriwa kuwa katika sikukuu ya mwaka huu, idadi ya wachina watakaotalii itazidi milioni 160. Miji inayopendelewa zaidi na watalii wa China ni Guangzhou, Beijing, Suzhou, Shenzhen, Shanghai, Hangzhou, Nanjing, Chengdu, Tianjin na Xi'an. Aidha utalii wa safari fupi na ya kati pia unafurahiwa na wachina, haswa bustani zenye mada maalumu zilizoko kwenye vitongoji vya miji zinawavutia watalii wengi. Kati ya njia za usafiri zinazotumika, reli ya mwendo kasi imechaguliwa zaidi na watalii wa China.

  Licha ya utalii wa ndani, wachina wengi pia wametalii nchi za nje. Ripoti iliyotolewa na idara ya utalii inakadiria kuwa, katika mapumziko ya sikukuu ya Mei Mosi ya mwaka huu, idadi ya wachina watakaotalii nchi za nje itaongezeka kwa karibu asilimia 8, na Thailand, Japan, Singapore, Vietnam, Malaysia, Indonesia, Philippines zitakuwa na watalii wengi kutoka China. Bi. Ge Mu ni meneja wa shirika moja la utalii la China. anasema,

  "Kutokana na kurefushwa kwa mapumziko ya sikukuu ya Mei Mosi, tumepanga safari ya siku nne. Kama watalii wetu wakiwa na mapumziko ya siku zaidi ya 8, wataweza kutalii nchini Japan, na Thailand."

  Katika sikukuu ya Mei Mosi ya mwaka huu, miji mbalimbali ya China pia imeandaa shughuli nyingi za kusherehekea sikukuu hiyo. Mji wa Beijing utafanya maonesho 304 ya aina mbalimbali, huku mji wa Wuhan ukiandaa maonesho ya taa za rangi na safari ya usiku kwenye Mto Changjiang.

  Idara husika zinakadiria kuwa utalii utasababisha ongezeko la matumizi, haswa matumizi ya chakula na manunuzi. Mtafiti wa Kituo cha Utafiti wa Utalii cha Akademia ya Sayansi ya Kijamii ya China Bi. Song Rui amesema marekebisho ya mapumziko ya sikukuu ya Mei Mosi yatahimiza ukuaji wa uchumi wa sikukuu, na kuongeza matumizi ya kijamii. Anasema,

  "Mchango wa matumizi kwa maendeleo ya uchumi umezidi asilimia 50, na matumizi ya huduma pia yamechukua asilimia 50 ya matumizi yote ya wananchi. Matumizi ya huduma ni tofauti na kununua vitu, na yanachukua muda mrefu. Kama watu wakiwa na wakati wa kutosha, wataongeza matumizi ya huduma."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako