• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Klabu bingwa Ulaya- Barcelona ikiongozwa na Messi yaipigisha kwata Liverpool bila huruma

  (GMT+08:00) 2019-05-02 08:26:21

  Pamoja na kuwa Liverpool waliruhusu kufungwa goli kipindi cha kwanza dakika ya 25 na Luis Suarez katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya (UEFA Champions League) dhidi ya FC Barcelona, majogoo hao wa Anfiled wameonyesha uhai mkubwa kiasi cha kuielemea Barcelona ambayo ilikuwa nyumbani.

  Barcelona walionekana kuzidiwa zaidi na Liverpool katika eneo la kiungo lakini baadae Lionel Messi aliamua matokeo ya mchezo huo kwa kubadilisha hali ya hewa ghafla baada ya kufunga magoli mawili ya ushindi dakika ya 74 na 81 na kuufanya mchezo huo uliyochezwa usiku wa kuamkia leo kumalizika kwa Barcelona kupata ushindi wa bao 3-0.

  Matokeo hayo sasa yataifanya FC Barcelona isafiri hadi Anfield kutafuta sare, ushindi au kufungwa kwa chini ya magoli matatu ili waingie fainali,

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako