• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mbunge wa Uingereza atetea ushirikiano wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja"

  (GMT+08:00) 2019-05-02 17:55:01

  Mbunge wa Uingereza Bw. Faisal Rashid, ambaye pia ni mwenyekiti wa kikundi cha wabunge wa vyama tofauti cha pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na "njia ya uchumi ya China na Pakistan" anafuatilia ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na kutetea ushirikiano kati ya China, Uingereza na Pakistan kufuatia pendekezo hilo.

  Bw. Rashidi mwenye umri wa miaka 46 aliyeteuliwa kuwa mbunge wa baraza la chini la bunge la Uingereza mwaka 2017, ni mwanachama wa kamati ya biashara ya kimataifa ya bunge hilo. Anasema,

  "Mkutano wa kilele wa ushirikiano wa kimataifa wa pendekezo la 'Ukanda Mmoja, Njia Moja' uliofanyika hivi karibuni umepata mafanikio makubwa. Naona kuwa China imefanya ushirikiano zaidi na nchi nyingine katika mchakato wa maendeleo ya pendekezo hilo."

  Mwaka 2017, Bw. Rashidi alitembelea mji wa Guangdong nchini China, na kupata nafasi ya kuelewa pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" kwa kina zaidi. Alipozungumzia sauti tofauti katika machakato wa maendeleo ya pendekezo hilo, anaona kuwa hii ni hali ya kawaida. Amesema pendekezo hilo lilitolewa miaka 6 iliyopita, na bado kuna safari ndefu, anaamini kuwa uhusiano wa aina mbalimbali kuhusu pendekezo hilo utaiva zaidi baadaye.

  Bw. Rashidi ana asili ya Pakistan, na anatumai kuhimiza ushirikiano kati ya China, Uingereza na Pakistan kufuatia pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Mwezi Septemba mwaka jana, Bw. Rashidi aliunda kikundi cha wabunge wa vyama tofauti cha pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na "njia ya uchumi ya China na Pakistan" katika bunge la Uingereza, ili kuhimiza bunge hilo kuelewa zaidi pendekezo hilo, na kuzipatia kampuni za nchi hiyo nafasi za kujiunga na pendekezo hilo. Anasema,

  "Ushirikiano kati ya China, Uingereza na Pakistan ni muhimu, na nchi hizi zinapaswa kukaa pamoja na kuwa na uhusiano mzuri wa pande tatu. Nina asili ya Pakistan, nataka kuhimiza uhusiano kati ya China, Uingereza, na Pakistan. Hii ndiyo sababu yangu ya kuunda kikundi cha wabunge wa vyama tofauti cha pendekezo la 'Ukanda Mmoja, Njia Moja', na 'njia ya uchumi ya China na Pakistan'."

  Tarehe 30, mwezi Aprili, Bw. Rashidi aliendesha kongamano la kikundi hicho lenye kauli mbiu ya "Brexit na pendekezo la 'Ukanda Mmoja, Njia Moja'", ambalo lilishirikisha wajumbe karibu mia moja, wakiwemo kaimu balozi wa China nchini Uingereza Bi. Chen Wen, mjumbe maalumu wa serikali ya Uingereza anayeshughulikia pendekezo hilo Bw. Douglas Jardine Flint, waziri wa biashara ya kimataifa wa Uingereza Bw. Barry Gardiner, pamoja na wanasiasa na wafanyabiashara kutoka Pakistan.

  Kuhusu mpango wake katika siku zijazo, Bw. Rashidi amesema anapenda kuongeza mawasiliano na China, na kuendelea kusukuma mbele ushirikiano kati ya China, Uingereza na Pakistan kufuatia pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia moja."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako