• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ligi ya Ulaya (EUROPA LEAGUE) Arsenal wailaza Valencia, Chelsea yaambulia sare kwa Frankfurt

  (GMT+08:00) 2019-05-03 08:47:53

  Mshambuliaji wa Arsenal Alexandre Lacazette amefunga magoli mawili huku Arsenal ikitoka nyuma katika uwanja wa Emirates na kuilaza Valencia katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya ligi ya Ulaya. Hadi kipenga cha mwisho kinapulizwa, Arsenal wameibuka na ushindi wa magoli 3-1.

  Wakati huo huo, watoto wa darajani Stamford Chelsea the blues imetoka sare ya 1-1 na Eintacht Franfurt baada ya kiungo wake Pedro kuipatia timu yake bao la ugenini. Franfurt ilianza kupata bao kupitia mshambuliaji Luka Jovic ambaye alipata pasi nzuri kutoka kwa Filip Kostic.

  Sare hiyo inamaanisha kwamba Chelsea itakuwa timu ya kwanza kucheza mechi 16 za Europa League bila kushindwa, Arsenal wao sasa itaelekea Valencia kwa awamu ya pili siku ya Alhamisi ya wiki ijayo wakitumai kuzuia kushindwa kwa nusu fainali yao ya pili baada ya kuondolewa na Ateltico madrid mwaka uliopita.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako