• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 41 wafariki baada ya ndege kuwaka moto Moscow

    (GMT+08:00) 2019-05-06 09:04:59

    Kamati ya upelelezi ya Russia imethibitisha kuwa watu 41 wamefariki dunia na wengine 37 kuokolewa baada ya ndege ya abiria aina ya SSJ-100 waliyokuwa wakisafiria kuelekea mji wa Murmansk, kuwaka moto kabla ya kutua kwa dharura Jumapili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Sheremetyevo mjini Moscow.

    Ndege hiyo iliripotiwa kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Sheremetyevo saa 12 jioni kwa saa za huko na kutua kwa dharua kwenye uwanja huohuo baada ya kuzunguka kwenye anga ya Moscow kwa dakika 40.

    Kamati hiyo imefungua kesi ya jinai ya ukiukaji wa kanuni za usalama kwenye usafiri wa anga na kuanza uchunguzi wa ajali hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako