• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Man City yaendelea kupambana kutetea taji lake la Ligi Kuu ya England

  (GMT+08:00) 2019-05-07 08:26:52

  Klabu ya Man City ya England ambayo kwa sasa inapambana kutetea taji lake la Ligi Kuu ya England msimu wa 2018/2019, walicheza mechi yao muhimu na ya mwisho nyumbani dhidi ya Leicester City mechi ambayo ni muhimu kupata matokeo mazuri ili kujiweka nafasi nzuri ya kutetea taji lao la Ligi Kuu England. Man City wakiwa nyumbani wamefanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0 lililofungwa na nahodha wao Vincent Kompany dakika ya 70 akiwa nje ya 18 kwa shuti kali, hiyo ni baada ya ukuta wa Leicester City kuwa imara na kushindwa kupenya kirahisi kiasi cha kujikuta wakicheza dakika 69 bila kupata goli lolote. Leicester kama jana wangetoka sare wangewaharibia Man City ambao wameanza kusherehekea kimya kimya taji la EPL. Ushindi huo unawarudisha Man City kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu England wakiwa wamecheza michezo 37 sawa na Liverpool na wakiongoza kwa point 95 wakifuatiwa na Liverpool wenye point 94, wote wamesaliwa na mchezo mmoja kumaliza Ligi. Man City itakuwa ugenini dhidi ya Brighton na Liverpool itakuwa nyumbani dhidi ya Wolves huku akiiombea mabaya Man City wateleze ili watwae taji la EPL kwa mara ya kwanza baada ya miaka 29.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako