• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano wa pili wa viongozi wa Ujenzi wa teknolojia ya dijitali wa China wafunguliwa mjini Fuzhou

  (GMT+08:00) 2019-05-07 19:40:00

  Mkutano wa Pili wa Ujenzi wa teknolojia ya dijitali wa China umefunguliwa mjini Fuzhou, mkoani Fujian, na umeshirikisha makampuni kutoka mikoa na miji 31, ikiwemo Mikoa ya utawala maalumu ya Hong Kong, Macao na Taiwan, na kuonesha maendeleo yaliyopatikana nchini China katika ujenzi wa teknolojia ya dijitali.

  Kauli mbiu ya mkutano huo ni "kuhimiza msukumo mpya kwa njia ya upashanaji wa habari, kuhimiza maendeleo mapya kwa msukumo mpya, na kutafuta mafanikio mapya kwa maendeleo mapya." Jukwaa la ushirikiano linaloandaliwa kwenye mkutano huo kuhusu kuunganisha nguvu za dunia kuhimiza ujenzi wa teknolojia ya kidijitali wa China, limeshirikisha mashirika na makampuni kutoka nchi 5 zikiwemo Uingereza, Ufaransa, Marekani, Denmark na Israel.

  Jambo linalofuatiliwa sana na watu ni kwamba, majumba yote ya maonesho kwenye mkutano huo yanatumia teknolojia ya 5G. Mfanyakazi mmoja ameonekana akiendesha gari ambalo skrini yake imeonesha hali ilivyo barabarani. Mfanyakazi huyo amesema gari hilo linaendeshwa kwa kutegemea teknolojia ya 5G:

  "Gari hili linaweza kufikisha takwimu mbalimbali za mfumo wa udhibiti, aina mbalimbali za vyombo vya upimaji, na usimamizi wa video hadi kwenye mtandao mkuu na hatimaye kwenye chumba cha uendeshaji."

  Kwenye mkutano wa baraza hilo, Ofisi ya habari ya mtandao wa Internet ya China imetoa ripoti kuhusu maendeleo ya ujenzi wa teknolojia ya kidijitali wa China. Naibu mkurugenzi wa ofisi hiyo Bw. Yang Xiaowei anasema:

  "Mwaka 2018 thamani ya uchumi wa dijitali ilifikia RMB trilioni 31.3, kiasi ambacho kinachukua asilimia 34.8 ya pato la ndani la taifa GDP."

  Umuhimu wa teknolojia ya kidijitali na upashanaji wa habari katika kuhimiza maendeleo yenye kiwango cha juu ya mkoa wa Fujian umeongezeka siku hadi siku, na thamani ya uchumi wa kidijitali ya mkoa huo ilifikia yuan trilioni 1.42, sawa na dola za kimarekani bilioni 212, kiasi ambacho kimechukua zaidi ya asilimia 30 ya GDP. Katibu wa Kamati ya chama cha Kikomunisti mkoani Fujian Bw. Yu Weiguo anasema:

  "Ujenzi wa teknolojia ya kidijitali mkoani Fujian umeleta fursa na msukumo muhimu. Tutafanya juhudi kuhimiza muungano wa kina wa upashanaji wa habari na utandawazi wa viwanda, na kuharakisha hatua ya kuendeleza uchumi wa kidijitali, kuhakikisha na kuboresha maisha ya watu kwa kupitia upashanaji wa habari, ili kuhimiza maendeleo yenye kiwango cha juu ya uchumi wa dijitali na eneo la kielelezo la ujenzi wa teknolojia ya dijitali nchini China."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako