• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kundi la Uchumi la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" limekuwa kundi kubwa la pili la uchumi duniani

  (GMT+08:00) 2019-05-08 18:26:59

  Tokea mwezi Mei mwaka huu, ripoti mbili za utafiti kuhusu Ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" zimefuatiliwa sana na watu. Moja ni Ripoti ya vigezo vya uwekezaji wa biashara wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" iliyotolewa na washauri mabingwa wa China na wa nchi za nje wanaoongozwa na Kituo cha mawasiliano ya uchumi cha kimataifa cha China

  Ripoti hii imeonesha kuwa kundi la uchumi la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" limezidi eneo la biashara huria la Amerika ya Kaskazini na kuwa kundi kubwa la pili la uchumi duniani likifuatia Umoja wa Ulaya, na faida zake za biashara zimeonekana. Ripoti nyingine imetolewa na kampuni ya inayojulikana ya utoaji wa tathmini ya Moody's na imesema, pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" limezisaidia nchi zinazotekeleza miradi mbalimbali kuongeza uwezo wao wa uzalishaji, kwa kupitia ujenzi wa miradi mikubwa ya miundombinu, na kutoa mchango kwa ajili ya mustakabali wa maendeleo ya uchumi katika nchi hizo.

  Ripoti ya vigezo vya uwekezaji wa biashara ya "Ukanda Mmoja, Njia Moja" imesema, thamani ya biashara ya kundi la uchumi la Pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" katika dunia nzima imeongezeka hadi asilimia 55.2 mwaka 2017. Mbali na hayo, thamani ya biashara kati ya wanachama wa kundi hilo pia imeongezeka kwa asilimia 13.4 katika thamani ya jumla ya biashara ya dunia nzima, na kuzidi eneo la biashara huria la Amerika ya Kaskazini, ikiwa ni sawasawa na asilimia 65 ya thamani ya biashara ndani ya Umoja wa Ulaya. Mtafiti wa suala hilo Bibi Zhang Monan anaona kuwa, kundi la uchumi la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" limekuwa sehemu muhimu zaidi ya kuvutia uwekezaji wa kigeni duniani.

  Ongezeko la biashara na uwekezaji ni chanzo muhimu katika kuhimiza kufufuka kwa uchumi duniani. Ripoti hiyo imefafanua kwa kutumia takwimu halisi kwamba, ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" umehimiza shughuli za biashara na uwekezaji kwenye sehemu na nchi zinazojiunga na pendekezo hilo, na pia kusaidia uchumi wa dunia kuondokana na matatizo.

  Ripoti ya utafiti ya kampuni ya Moody's imeonesha kuwa, Pakistan, Mongolia, Kazakhstan na Cambodia ni nchi zinazopata ongezeko kubwa zaidi la uchumi kutokana na miradi ya "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Rais wa kwanza wa Kazakhstan Bw. Nursultan Nazarbayev alipokuja Beijing kushiriki kwenye mkutano wa viongozi wa Baraza la Ushirikiano wa Kimataifa la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" alisema, nchi yake haina bandari, lakini ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" umeziwezesha reli 6 na barabara 11 kupita nchini humo, na kituo cha ushirikiano wa usambazaji wa bidhaa kilichojengwa na Kampuni ya China kimeifanya Kazakhstan kupata mlango wa kuingia bahari ya Pasifiki.

  Kama rais Xi Jinping wa China alivyosema "umuhimu wa ujenzi wa pamoja wa 'Ukanda Mmoja, Njia Moja' ni kuunganishana na kuwasiliana. Tunatakiwa kujenga uhusiano wa kiwenzi wa kuunganishana na kuwasiliana katika dunia nzima, ili kupata maendeleo na ustawi kwa pamoja."

  Katika Mkutano wa pili wa viongozi wa Baraza la Ushirikiano wa kimataifa la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" uliomalizika hivi karibuni, viongozi wa nchi mbalimbali walitoa taarifa ya pamoja wakisifu kwa kauli moja maendeleo yaliopatikana na fursa muhimu zinazoletwa kutokana na ushirikiano wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na kutia nia imara ya kushirikiana katika ujenzi huo. Ripoti zilizotolewa na Kituo cha mawasiliano ya uchumi cha kimataifa cha China na kampuni ya Moody's zimethibitisha kwamba, kundi la uchumi la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" linaloshikilia kanuni ya kujadiliana, kujenga na kunufaishwa kwa pamoja linatazamiwa kutoa mchango mpya kwa ajili ya sehemu na nchi zinazojiunga na pendekezo hilo na dunia nzima.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako