• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Wakulima kujaribu aina mpya ya kahawa

    (GMT+08:00) 2019-05-08 20:51:38

    Watafiti kwenye halmashauri ya kilimo nchini Rwanda imetangaza mipango ya kutoa aina 9 ya mbegu za kahawa kwa wakulima ili kufanyia majaribio.

    Halmashauri hiyo inasema aina hizo mpya zinatarajiwa kuwa na mavuno ya juu.

    Mtafiti kwenye halmashauri hiyo bwana Simon Martin Mvuyekure, amesema tayar wamefanyia majaribio mbegu hizo mpya katika kituo chao na matokeo yake ni ya kuridhisha.

    Amesema kwa kawaida wakulima huvuna kilo tano hivi za mbuni kutoka mti mmoja wa kahawa lakini aina hiyo mpya kwa jina F1 inatarajiwa kuwaletea hadi kilo 18.

    Taakwimu zinaonyesha kuwa uzalishaji wa kahawa nchini Rwanda kati ya Juni 2018 na 2018 uliongezeka kwa asilimia 19.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako