• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Ligi ya Mabingwa Ulaya- Hatimaye Tottenham waifuata Liverpool fainali

    (GMT+08:00) 2019-05-09 08:01:44
    Mchezo wa mwisho wa nusu fainali ya klabu bingwa Ulaya imepigwa jana baina ya wenyeji Ajax ya Uholanzi dhidi ya Tottenham ya Uingereza. Tottenham imetoka nyuma na kuilaza Ajax ugenini na kutinga fainali ya michuano hiyo ambapo sasa itakutana na Majogoo wa Anfield Liverpool kwenye mchezo wa fainali.

    Lucas Noura amefunga bao la ushindi dakika ya 96 ya mchezo na kusaidia timu yake kuwalaza miamba hiyo ya Uholanzi kwa mabao 3-2.

    Hii itakuwa ni fainali ya pili inayoziweka pamoja timu mbili za Uingereza, baada ya Manchester United kuipiku Chelsea kupitia mikwaju ya Penalti mjini Moscow mwaka 2008.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako