• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ripoti ya utafiti ya Marekani yaona hatari ya madeni ya "Ukanda Mmoja, Njia Moja" imekuzwa

    (GMT+08:00) 2019-05-09 09:41:07

    Taasisi ya utafiti wa masuala ya China na Afrika katika Chuo Kikuu cha The Johns Hopkins nchini Marekani na kampuni ya ushauri ya Marekani Rohdium zimetoa ripoti zikisema, hatari ya madeni ya pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" huwa inakuzwa.

    Ripoti ya utafiti iliyotolewa na Taasisi ya utafiti wa masuala ya China na Afrika katika Chuo Kikuu cha The Johns Hopkins inasema, hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2017, nchi zipatazo 17 zenye kipato cha chini zimekuwa au zinakabiliwa na "msukosuko wa madeni", au zinapata shida katika kulipa madeni ya umma. Taasisi hiyo imetafiti nyaraka za madeni zilizoandaliwa kwa ajili ya nchi hizo na kugundua kuwa, wengi wa watoaji mikopo wa nchi hizo sio China. Kwa mfano, Benki ya Mikopo ya Uswisi ilitoa mikopo mingi nchini Msumbiji, na kampuni ya nishati, kilimo na madeni ya Glencore International ya Uswisi nayo imetoa mikopo mingi kwa Chad.

    Mkurugenzi wa taasisi hiyo Deborah Brautigam ametoa makala katika gazeti la New York Times akisema "Ukanda Mmoja, Njia Moja" sio "diplomasia ya mtego wa madeni", bali ni pendekezo la utandawazi lenye umaalum wa kichina.

    Bi. Brautigam ametolea mfano wa bandari ya Hambantota nchini Sri Lanka, akisema kabla ya kuuza bandari hiyo mwaka 2016, Sri Lanka ilikuwa na deni la kigeni la dola za kimarekani bilioni 46.5, na kati yao asilimia 10, sawa na dola za kimarekani bilioni 4.6 ilitoka China. Hivyo, suala la madeni la Sri Lanka halikusababishwa na China.

    Bi. Brautigam pia amenukuu ripoti ya utafiti wa masuala ya eneo la Latin Amerika na Caribbean na China iliyotolewa na kituo cha utafiti wa sera za maendeleo duniani cha Chuo Kikuu cha Boston akisema, China imetoa mikopo mingi katika nchi na sehemu chache katika eneo la Latin Amerika na Caribbean, na mikopo inayotolewa na China haizidi kikomo cha madeni endelevu kilichowekwa na Shirika la Fedha la Kimataifa.

    Wakati huohuo, ripoti iliyotolewa hivi karibuni na kampuni ya ushauri ya Marekani Rhodium imesema, itakuwa na uwiano zaidi kwa wakopaji na wakopeshaji baada ya China na baadhi ya nchi zinazoshiriki kwenye ujenzi wa pamoja wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" kufanya mazungumzo upya.

    Ripoti hiyo imefanya utafiti juu ya kesi zaidi ya 40 kuhusu China kufanya mazungumzo mapya na nchi za "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na kuonyesha kuwa, China ina uchumi mkubwa, lakini matokeo ya mazungumzo hayo yanazinufaisha zaidi nchi zilizopokea mikopo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako