• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SIDO yachagiza utekelezaji wa programu bidhaa moja wilaya moja

    (GMT+08:00) 2019-05-09 20:28:59
    Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo nchini Tanzania (SIDO) limesema mwitikio wa mikoa katika kutekelezaji Programu ya wilaya moja bidhaa moja (ODOP) utachochea uzalishaji wa bidhaa zinazotokana na mazao ya kilimo na mifugo nchini humo.

    Mkurugenzi Mkuu wa SIDO, Prof.Sylvester Mpanduji, amesema utekelezaji wake umeanza kwa mafanikio baadhi ya mikoa.

    Alisema kuwepo kwa ODOP kumeamsha hali kwa wananchi kujikita katika uzalishaji zaidi hali inayochochea ukuaji wa uchumi na kufanikisha azma ya serikali ya kufikia uchumi wa kati na viwanda ifikapo 2025 kwa vitendo.

    Ameongeza kuwa jukumu la SIDO katika program ya ODOP ni kuhakikisha viwanda vinajengwa katika kila wilaya kwa lengo la kuzalisha bidhaa moja itakayochaguliwa na wilaya husika ambapo uhamasishaji utafanywa katika uzalishaji wa mazao ili yatumike kama malighafi ya kiwanda na kuzalisha bidhaa.

    Prof.Mpanduji amewataka Watanzania kutumia programu hiyo kwa kuwa mafanikio yake ni makubwa katika kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla kama kutakuwa na utayari katika kufanya kazi kwa pamoja.

    Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Uwekezaji wa SIDO, Shoma Kibende, alisema ODOP imefanikiwa kwa kiwango kikubwa kutokana na mwitikio wa kila wilaya katika programu hiyo ambayo imekuwa mkombozi wa mazao ya wakulima.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako