• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: UEFA Europa League- Uingereza yaandika historia mpya ya soka Ulaya, Chelsea na Arsenal kukutana fainali

  (GMT+08:00) 2019-05-10 08:34:19

  Wakati Liverpool na Tottenham zimemaliza majukumu yao ya kufikia fainali za klabu bingwa Ulaya. Jana timu ya Chelsea ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani Stamford Bridge imeikaribisha Entracht Frankfurt kwa mchezo wa marudiano ya nusu fainali ya ligi ya Ulaya,

  kipa Kepa Arrizabalaga na mshambuliaji Edin Hazard wa Chelsea wameiwezesha timu yao kutinga fainali kwa ushindi wa penalti 4-3 kufuatia sare ya jumla ya magoli 2-2 ndani ya dakika 210 kwenye mechi mbili za nyumbani na ugenini.

  Nao washika bunduki wa jijini la London Arsenal, wao walikuwa ugenini uwanja wa Mestalla walipovaana na Valencia. Mshambuliaji wa kimataifa wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang alipiga hat trick kwa mabao yake dakika ya 11, 69 na 88 ikiwalaza wenyeji Valencia kwa bao 4-2.

  Goli la Valencia lilifungwa na Kevin Gamiero dakika ya 11 na 58. Kwa matokeo hayo, Arsenal inakwenda fainali kwa ushindi wa jumla ya magoli 7-3. Hivyo Arsenal itakutana na Chelsea katika mchezo wa fainali hizo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako