• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa wahimiza kuongeza ushirikiano kati ya sekta za umma na binafsi katika sekta ya fedha ya Afrika

    (GMT+08:00) 2019-05-10 09:36:30

    Katibu mtendaji wa kamati ya uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa ECA, Vera Songwe amesisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya sekta za umma na binafsi PPP ili kukuza sekta ya fedha barani Afrika.

    Bibi Songwe amesema, ni muhimu kuelewa jinsi ya kutumia misaada ya kimaendeleo na rasilimali za umma au binafsi na uwekazaji mpya wakati wa kukabiliana na matatizo ya ushirikiano wa sekta za umma na binafsi za mashirika mbalimbali ili kuongeza matumizi yao katika maeneo muhimu, yakiwemo ya maji na usafi wa mazingira.

    Pia amesema, hivi sasa, hatari nyingi za miradi ya PPP bado ziko kwenye sekta ya umma. Hivyo amesisitiza kuwa inapaswa kubadilisha uwiano huo na kugawa hatari hizo kati ya sekta hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako