• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Kenya aongezewa mshahara

    (GMT+08:00) 2019-05-10 19:46:49

    Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake Dkt William Ruto watapata nyongeza ya mshahara ya asilimia 3.9.

    Nyongeza hiyo iliondolewa 2017 wakati wa uchaguzi, pamoja na nyongeza ya viongozi wengine wakuu serikalini kukabiliana na ongezeko la mzigo wa mishahara nchini.

    Kulingana na stakabadhi rasmi kutoka kwa Hazina Kuu, mshahara wao utaongezwa kutoka Sh36.6 milioni kwa mwaka hadi Sh38 milioni.

    Baada ya kukatwa kwa nyongeza hiyo, mshahara wa rais ulipungua kutoka Sh1.65 milioni hadi Sh1.44 milioni na naibu wake kutoka Sh1.4 milioni hadi Sh1.23 milioni.

    Nyongeza hiyo imepangiwa kutekelezwa wakati Hazina ya Fedha inalenga kuongeza kiwango cha fedha za maendeleo na huduma za kimsingi kama vile usalama, afya na elimu.

    Lakini kumekuwa na changamoto ya uokotaji wa mapato, hali ambayo ililazimisha Hazina ya Fedha kutathmini bajeti yake.

    Viongozi hao wawili pia watapata marupurupu ya Sh15.2 milioni kwa mwaka, mwaka wa kifedha unaoanzia Julai 2019.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako