• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TPAWU walia michango NSSF

    (GMT+08:00) 2019-05-10 19:47:09
    Chama cha Wafanyakazi wa Mashambani na Kilimo nchini Tanzania (TPAWU), kimeiomba serikali kuingili kati tatizo la kukatwa fedha na waajiri wao za Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), ambapo fedha hizo haziwasilishwi kwa wakati kwenye mfuko.

    Mwenyekiti wa (TPAWU) Tawi la Relongo Estate Wilaya ya Siha, Rashid Mswaki, alifafanua waajiri hao wamekuwa wakiwakata fedha hizo kwa ajili ya mifuko mbalimbali ya kijamii ikiwamo NSSF, ili hali waajiri wao hawaziwasilishi fedha hizo kwa wakati.

    Mswaki aliiomba serikali na uongozi wa TPAWU iwasaidie kutatua tatizo hilo ambalo limegeuka kuwa mwiba kwa ustawi wa kiuchumi kwa kazi zao na familia zao.

    Kwa upande wake, mwenyekiti wa TPAWU, tawi la TPC Bw Elius Mashmba, amesema changamoto kubwa iliyoko kwa wafanyakazi wanapoumwa wakienda kutibiwa hospitalini hawapati huduma hiyo kutokana na fedha wanazokatwa kutokuwasilishwa na waajili wao.

    Naye Suzan Nkini, mwenyekiti wa vijana TPAWU Kanda ya Kilimanjaro, ameiomba serikali isaidie kuzibana taasisi ambazo zinashindwa kupeleka michango ya wafanyakazi wao kwa wakati.

    Waajiri wametakiwa kuendelea kuwapa fursa wafanyakazi wao kwenda kupata ujuzi ili kujenga mahusiano mazuri baina ya wafanyakazi na waajiri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako