• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UCHAMBUZI: Kutilia maanani yanayofuatiliwa na kila upande ni msingi wa kutatua mikwaruzano ya kiuchumi na kibiashara

    (GMT+08:00) 2019-05-11 10:36:08

    Mazungumzo ya duru ya 11 ya mambo ya kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani yalimalizika Ijumaa huko Washington. Mwakilishi wa China katika mazungumzo hayo ambaye pia ni naibu waziri mkuu Bw Liu He aliwaambia wanahabari kuwa, pande mbili zilifanya maongezi na kupeana ushirikiano, na kwamba mazungumzo hayakuvunjika ila tu yalikumbwa na matatizo madogo, hali ambayo ni ya kawaida na isiyoweza kuepukika katika mazungumzo. Aliongeza kuwa, China ina imani na mazungumzo ya siku za usoni.
    Si ajabu kupata matokeo hayo. Kwani mazungumzo hayo yalikuwa yameendelea kwa duru 11 toka mwezi Februari mwaka jana. Pamoja na kwamba maendeleo muhimu yalipatikana, lakini baadhi ya mambo yalijirejea mara kadhaa. Kabla ya duru hiyo ya 11 ya mazungumzo, watu walihofia huenda mazungumzo yangevunjika kutokana na kauli ya Marekani kuhusu kupandisha kiwango cha ushuru wa forodha. Katika hali hii, ujumbe wa China ulikwenda Washington kama ilivyopangwa, ukionyesha udhati na uwajibikaji.
    Lakini Marekani iliinyooshea kidole China kwa kutaka kujadiliana tena baadhi ya yaliyomo kwenye makubaliano, ikilenga kuifanya China ibebe lawama za kushindwa kwa mazungumzo. Hatua hiyo si haki.
    Hadi hivi leo, Marekani inasisitiza tu kuwa China inapaswa kuiridhisha matakwa yake, huku ikiendelea kukwepa kutaja kama Marekani nayo pia inapaswa kuiridhisha China. Ni kinyume na kanuni ya kufanya mazungumzo, pia ni sababu muhimu ya kushindwa kwa duru hiyo ya mazumgumzo.
    China haitarudi nyuma katika masuala yanayofuatiliwa nayo. Suala la kwanza ni kufuta kabisa ushuru wa forodha ulioongezwa, na kurejesha hali ya kawaida ya kibiashara. Kwani ushuru wa forodha ni mwanzo wa mikwaruzano hiyo, hakika unapaswa kufutwa kabisa endapo makubaliano yatafikiwa.
    Inasikitisha kuona kuwa vita vya kibiashara kati ya China na Marekani vinaendelea kupanda ngazi, hata hivyo China imezoea hali kama hiyo. Katika kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja, Marekani ilikuwa inaendelea kupandisha kiwango cha ushuru wa forodha, uchumi wa China uliathirika kwa kiasi, lakini takwimu zimethibitisha kuwa, China ina uwezo wa kudhibiti na kukabili athari hizo. Katika miezi mitatu ya mwanzo mwaka huu, uchumi wa China uliongezeka kwa asilimia 6.4. Shirika la fedha la kimataifa IMF limerekebisha makadirio yake juu ya ongezeko la uchumi wa China mwaka huu kutoka asilimia 6.2 hadi asilimia 6.3. Hivi majuzi mwekezaji maarufu wa Marekani Bw Warren E. Buffett alieleza kuridhishwa na uwekezaji wake nchini China, akisema anapanga shughuli kubwa zaidi katika miaka 15 ijayo.
    Habari zinasema, maofisa wa mambo ya kiuchumi na kibiashara kutoka China na Marekani wataendelea na mazungumzo hapa Beijing. Hii inaonyesha kwamba, pande hizo mbili zinatambua kanuni na msingi wa kila upande, pia zinatamani kuendelea na mazungumzo ili kutatua masuala.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako