• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mtaalamu wa Marekani asema Marekani haipaswi kuweka vikwazo dhidi ya Huawei

  (GMT+08:00) 2019-05-12 17:46:50

  Mwanzilishi wa maabara ya vyombo vya habari vya chuo cha Teknolojia cha Massachusetts MIT Bw. Nicholas Negroponte hivi karibuni ameandika makala akisema sera za mawasiliano ya habari zinapaswa kufuata kigezo cha bila kupendelea, na wala si masuala ya siasa za kijiografia. Amesema Marekani haipaswi kuweka vikwazo dhidi ya kampuni ya Huawei ya China, inapaswa kuikaribisha ili kuhimiza mtandao wa kidijitali wa Marekani kuwa usalama zaidi na kujiendeleza zaidi.

  Bw. Negroponte amesisitiza kuwa, njia nzuri zaidi ni kukagua alama za software za makampuni yote ya kutoa huduma kwenye mtandao wa Marekani. Ili kuinua hadhi yake ya uongozi katika sekta ya teknolojia duniani, Marekani inapaswa kushirikiana na makampuni ya teknolojia na maabara zao, na kuunda kigezo kimoja kisicho na upendeleo sokoni, ambacho kitaamua kama teknolojia za kampuni hiyo zinaaminika au la.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako