• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Chama tawala cha ANC cha Afrika Kusini chashinda katika uchaguzi mkuu

  (GMT+08:00) 2019-05-12 20:53:35

  Tume huru ya uchaguzi ya Afrika Kusini imetangaza matokeo ya upigaji kura, na chama tawala cha ANC kimeshinda katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2019.

  Matokeo hayo yanaonesha kuwa chama cha ANC kitapata viti 230 kati ya viti 400 katika bunge la taifa la Afrika Kusini, chama cha muungano cha demokrasia cha Afrika Kusini kitapata viti 84 na chama cha EFF kitapata viti 44.

  Upigaji kura wa uchaguzi mkuu wa Afrika Kusini ulianza tarehe 8 mwezi Mei, na vyama 48 vilishiriki kugombea viti 400 kwenye bunge la taifa la Afrika Kusini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako