• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yafanya maandalizi kwa pande zote katika kukabiliana na mgogoro wa kibiashara na Marekani

    (GMT+08:00) 2019-05-13 08:36:38

    Baada ya Marekani kuongeza ushuru dhidi ya bidhaa za China zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 200 zinazouzwa nchini humo kutoka asilimia 10 hadi 25, imetishia tena kuanzisha utaratibu wa kuongeza ushuru kwa asilimia 25 kwa bidhaa nyingine za China zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 325, na kutangaza orodha za bidhaa hizo hivi karibuni. Wakati huo huo, raundi ya 11 ya mazungumzo ya ngazi ya juu ya uchumi na biashara kati ya China na Marekani imemalizika, na pande mbili zimekubaliana kuendelea na mazungumzo.

    Hali hii imeonesha kuwa Marekani inaendelea na jaribio la kuiwekea shinikizo China, huku ikidai faida kubwa kwenye mazungumzo. Lakini tukichambua kwa makini msimamo uliotolewa na naibu waziri mkuu wa China na kiongozi wa ujumbe wa mazungumzo ya kiuchumi ya pande zote kati ya China na Marekani Bw. Liu He, baada ya raundi ya 11 ya mazungumzo kati ya pande hizo mbili, Marekani inapaswa kutambua kuwa China kamwe haitasalimu amri juu ya ufuatiliaji wake tatu muhimu: kufuta ushuru wote ulioongezwa; takwimu kuhusu manunuzi ya kibiashara zinatakiwa kuendana na hali halisi; na kuhakikisha maelezo yenye uwiano kwenye nyaraka zinazofikiwa kati ya pande hizo mbili.

    Bila kujali Marekani inaweza kutoa shinikizo gani dhidi ya China, haikufanikiwa, haifanikiwi na hakika haitafanikiwa katika siku za baadaye. Mazungumzo ya uchumi na biashara kati ya pande hizo mbili katika mwaka uliopita, yamepata maendeleo muhimu na pia yalirudi nyuma mara kadhaa, lakini China siku zote imekuwa na nia njema ya kuyasukuma mbele. Kwani inafahamu vizuri kwamba hakutakuwa na mshindi katika vita ya biashara, na hatua za kuongeza ushuru wa forodha haitasaidia pande zote mbili wala dunia nzima, na ushirikiano ni chaguo sahihi na pekee kati ya pande hizo mbili. Lakini ushirikiano huo unafanyika kwa masharti ya kukidhi ufuatiliaji muhimu wa China, na China haitakubali Marekani kuuchochea na kuukiuka.

    China itapinga kithabiti kama Marekani inashikilia nia ya kuendelea kuongeza ushuru. Katika mwaka uliopita, China imeshinda mitihani mbalimbali katika migogoro hiyo ya kibiashara, huku uwezo wake wa kukabiliana na mashinikizo ukiongezeka. Kwani China imetambua wazi kwamba, hatua ya Marekani ya kuongeza ushuru ni kuchezea kamari ya hatari ya kujiharibia, ambayo imekwenda kinyume na maoni ya raia na hakika itashindwa. Ripoti ya utafiti iliyotolewa mwezi Februari na Kampuni ya ushauri ya "wenzi wa biashara wa dunia nzima" ya Marekani imeonesha kuwa, Marekani ikiongeza ushuru kwa asilimia 25 kwa bidhaa za China zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 250 zinazouzwa nchini humo, itapoteza nafasi laki 9.34 za ajira, wastani wa matumizi ya fedha ya familia za wamarekani zenye watu wanne, utaongezeka kwa dola za kimarekani 767 kwa mwaka; ikiwa Marekani itakapoongeza ushuru kwa bidhaa nyingine za China zenye dola za kimarekani bilioni 325, itazidi kupoteza nafasi milioni 2.1 za ajira kwa mwaka, na wastani wa matumizi ya fedha ya familia za Marekani zenye watu wanne yatazidi kuongezeka kwa dola 2,000 kwa mwaka.

    Ukiwa upande wa kulazimishwa kujibu vita hiyo ya kibiashara, bila shaka uchumi wa China utakabiliwa na shinikizo, lakini shinikizo hilo linadhibitika. Kutokana na muundo wa uchumi, thamani ya matumizi inachangia asilimia 76.2 ya ongezeko la pato la ndani la China, huku thamani ya uuzaji wa bidhaa nje ikipungua hadi asilimia 17.9, na mahitaji ya soko la ndani yamekuwa msukumo muhimu wa China katika kukabiliana na hali isiyotarajiwa ya mazingira ya nje.

    Katika upande wa biashara, katika miezi minne ya mwanzo ya mwaka huu, thamani ya biashara kati ya China na Marekani imepungua kwa asilimia 11.2, ile ya uuzaji wa bidhaa nje imepungua kwa asilimia 4.8, thamani ya uagizaji wa bidhaa kutoka Marekani imepungua kwa asilimia 26.8, hali ambayo imeonesha kuwa bidhaa zinazouzwa na Marekani nchini China zina mbadala. Wakati huo huo, urari wa biashara kati ya China na Marekani umepanuka kwa asilimia 10.5, hali ambayo imeonesha kuwa kuongeza ushuru hakuwezi kutatua tatizo la kutokuwepo kwa uwiano wa kibiashara kati ya pande hizo mbili, badala yake inaweza tu kuongeza gharama kwa wateja wa Marekani.

    Mbali na hayo, katika miezi minne iliyopita, thamani ya biashara kati ya China na Marekani ilipungua hadi asilimia 11.5 katika thamani ya jumla ya biashara kati ya China na nchi za nje, huku thamani hiyo na wenzi muhimu wa biashara zikiwemo Umoja wa Ulaya na Umoja wa nchi za Asia Mashariki ikidumisha ongezeko la kasi, na ile kati ya China na nchi zinazojiunga na Pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" imeongezeka kwa asilimia 9.1, kiasi ambacho kimezidi kwa asilimia 4.8 kuliko kiwango cha jumla cha biashara na nje na China. Hali hiyo imeonesha kuwa idadi ya wenzi wa biashara na nje ya China imeongezeka, huku uwezo wake wa kukabiliana na shinikizo ukizidi kuongezeka. Hii inamaanisha kuwa hata kama Marekani itaongeza ushuru kwa bidhaa zote za China zinazouzwa nchini humo, China itaweza kuhamishia biashara yake na Marekani katika nchi nyingine, kwa njia ya kurekebisha muundo wa soko la kimataifa.

    Hivi sasa kipaumbele cha China ni kushughulikia kwa makini mambo yake, kuendelea na mageuzi, kupanua ufunguaji mlango ili kutimiza maendeleo yenye ubora wa hali ya juu. Bila ya kujali Marekani itachukua hatua gani, China iko tayari kukabiliana nayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako